Kamati ya Elimu na Afya imekagua Miradi ya maendeleo tarehe 28/07/2025,Miradi iliyokaguliwa na Wataalamu hao ni Zahanati ya Nkuyu,Zahanati ya Ngana, Nyumba Moja Kwa mbili(Two in One) ya Walimu katika Shule ya Sekondari Ibanda na Ujenzi wa Nyumba za watumishi na ukamilishaji wa Madarasa katika Shule ya Wasicha Mbeya girls iliyopo Kata ya Busale.
Katika ukaguzi huo Mkurugenzi Mtendaji Adv Luhala amemuagiza Afisa Mtendaji wa Kata ya Nkuyu kuhakisha Zahanati ya Nkuyu inakamilika Kwa wakati.Hakuna sababu ya kuchelewesha mradi maana fedha ya mapato ya ndani ipo imetengwa Million 30 za kumalizia shughuli ya ujenzi.(Alisema Adv Luhala)
Aidha Adv Luhala kwenye mradi wa Nyumba Moja Kwa mbili alimuagiza fundi kukamilisha Nyumba hiyo kwani Kila kitu kipo. Kupitia mapato kutoka Serikali Kuu kiasi Cha Shilingi Million Mia Moja (100) zimeletwa Kwa mpango wa Mradi wa SEQUIP.
Ujenzi wa Shule ya Wasichana Mbeya(Mbeya girls) awamu ya pili,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kyela Adv Florah A.Luhala,ameridhishwa na idadi ya Mafundi aliowakuta wakiendelea na kazi katika Mradi huo.
Adv Luhala amewaambia mafundi hao wamalizi kazi walizopewa Kwa wakati sahihi na Kwa ubora unaokubalika,Awamu hii ya pili hapa kupitia Mradi wa SEQUIP Serikali ya Mama imeleta Billion Moja na Million mia Moja(1,100,000,000) ( Alisema Adv Luhala)
Aidha aliendelea kuambia mafundi waendelee kufanya kazi Kwa juhudi na Ubora unaokubarika,ili waendelee kuaminiwa na kupewa kazi nyingine kwani Serikali ya awamu ya sita imeleta fedha nyingi za Miradi,hivyo fundi atakaefanya kazi vizuri atapewa Miradi mingine.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa