Mkurgenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, ndugu Ezekiel H. Magehema amefanya kikao kazi na watumishi wote wa halmashauri ya wilaya ya Kyela lengo kubwa ni kutaka kusikiliza kero za watumishi hao na kuzipatia ufumbuzi.
Kikao hicho cha wafanyakazi kimefanyika leo tarehe 17/03/2023, katika ukumbi wa mikutano, Na kimejumuisha watumishi kutoka kila Idara ikiwa ni pamoja na wale wanaotoka katika kata na vijiji.
Pamoja na mambo mengi aliyoyaongea pia, Mkurugenzi mtendaji amewasisitiza watumishi wote kuheshimu kazi, Ikiwa ni pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo, kuwaheshimu watumishi wanaowaongoza.
Aidha amewataka watumishi, kuwa na bajeti nzuri ya matumizi ya mshahara wanaoupata, Pia amewaonya watumishi kuachana na ulevi na anasa zisizo na maana ili kijiletea maendeleo chanya.
Kwa upande wao watumishi wameweza kuuliza kuhusiana na upandishwaji wa madaraja ya mishahara pamoja na ulipwaji wa madeni, ambapo majibu yametolewa kwa ufasaha ndani ya kikao hicho.
Mwisho amewataka wakuu wa Idara na Vitengo kuendelea kuzipokea kero na kuwasikiliza wasaidizi wao punde wanapowahitaji ili kuongea nao katika ofisi zao ili kuleta mahusiano bora katika kazi.
Akitoa neno la shukrani Afisa kilimo Eng. Arnod Bachubila amemshukuru mkurugenzi mtendaji kwa kufanya kikao cha wazi na watumishi, lakini pia ameshirikisha vyama vya wafanyakazi na kuweka mambo yote bayana, ambapo kila Mtumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kyela amepata mwangaza wa kila alichotaka kukisikia kutoka kwa viongozi wake.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa