Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Josephine Manase ameongoza mkutano wa mwaka wa Idara ya Afya na Lishe katika ukumbi wa Palazo uliopo Kata ya Matema tarehe 31.7.2025.
Lengo la mkutano huo ni kufanya tathimini ya kazi Kwa mwaka uliopita,kuonesha mafanikio na changamoto zilizopatikana pamoja na kuweka mikakati ya kuboresha huduma za Afya na kuhakikisha mwananchi anapata huduma bora.
Mkutano huo umeambatana na ugawaji tuzo kwa viongozi wa Afya, Kata zilizofanya vizuri katika usafi, vituo vya afya vilivyofanya vizuri kwenye afua za Afya pamoja na kutoa shukrani kwa wadau mbalimbali wa Afya.
Akifungua mkutano Mhe .Manase ,amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya Afya, kama ujenzi wa zahanati na vituo vya afya ili kuhakikisha Wananchi wanapata huduma ya Afya wakati wowote.
Sambamba na hayo Mkuu wa Wilaya amewataka viongozi ngazi ya Kata kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya umuhimu wa vyoo na namna ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko pamoja na kutoa takwimu za usafi wa mazingira kwa wataalamu wa Afya.
Mhe.Manase amewaasa wafawidhi kutumia mfumo tangu anapofika mgonjwa kutibiwa hadi mwisho wa Matibabu yake, pia amewaagiza wafawidhi hao kuwa ifikapo tarehe 30/08/2025 wote wawe wanatumia Mfumo katika kutoa huduma za Matibabu.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa