Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Juma Zuberi Homera ameongoza mikutano wa Baraza la hoja katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 17.6.2025.
Akizungumza kwenye Baraza hilo Mhe. Mkuu wa Mkoa amewapongeza Wah.Madiwani kwa usimamizi mzuri wa mapato kwani mpaka sasa Halmashauri imefanikiwa kukusanya Tsh.bilioni 8.7 sawa na 125%.
Mhe.Homera amewaagiza Wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi waliowasilisha hoja kuzifanyia kazi hoja zao kwa wakati uliopangwa.
Aidha Mhe.Homera amewaasa Wataalamu kusimamia vyema fedha za Umma zilizopangwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ili Wananchi waweze kupata huduma kupitia miradi hiyo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa