Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Zuberi Homera, amegawa pikipiki 368 kwa niaba ya Mkoa wa Mbeya, ikiwa pikipiki 331 kwa maafisa Ugani na pikipiki 37 kwa watendaji wa kata, zoezi lililofanyika katika wilaya ya Kyela tarehe 21/02/2023.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa pikipiki hizo Mheshimiwa Mkuu wa mkoa amesema, Kwa maafisa wote na watendaji kata waliokabidhiwa pikipiki, wakazifanyie kazi iliyokusudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ili zilete tija kwa maendeleo ya wananchi.
"Twende tukafanye kazi ili tusimwangushe Rais wetu, na tuonekane tumetekeleza kwa vitendo Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa mwaka 2020/2025" Amesema Mhe. Juma Zuberi Homera.
Pamoja na hayo mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amewataka maafisa ugani wote kwenda kusimamia kilimo na kufanya uzalishaji wenye tija, hasa katika zao la Mchikichi na mpunga kwa wilaya ya Kyela kwani mazao hayo yanalimwa kwa wingi hapa wilayani Kyela.
Kwa upande wa watendaji wa kata, Mheshimiwa Juma Zuberi Homera amewataka kwenda kuzitumia pikipiki hizo kwa kukusanya mapato na kuongeza asilimia ya mapoto yaliyokusudiwa katika kila wilaya.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa mkoa ametoa pongezi nyingi kwa wilaya ya Chunya kwa kukusanya 87% ya mapato hadi kufikia tarehe 19/02/2023, Pongezi kwa wilaya ya Kyela kwa kukusanya 71% ya mapato ambapo wilaya ilikusudia kukusanya mapato ya shilingi bilioni 4 lakini hadi sasa wilaya imekusanya bilioni 3, pongezi nyingine zilitolewa kwa halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa ukusanyaji wa 66% hadi kufikia sasa, amesema anaamini kwa kupitia pikipiki hizi mapato yataongezeka zaidi na kuvunja mafanikio ya mwaka wa fedha uliyopita.
Pia Mheshimiwa Homera ametoa shukrani zake za dhati kwa uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela kwa kumpa nafasi ya kuzigawa pikipiki hizo kwa wilaya na kwa niaba ya mkoa mzima.
Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Josephine Keenja Manase ametoa shukrani zake za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuipatia wilaya ya Kyela pikipiki 49, na amewataka Maafisa wote na watendaji wa kata waliokabidhiwa pikipiki hizo kuzifanyia kazi ili ziweze kuleza maendeleo yenye tija kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Josephine Keenja Manase akiongea na maafisa Ugani na Watendaji Kata katika zoezi la ugawaji wa pikipiki
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkoni amewataka maafisa ugani na watendaji kata waligawiwa pikipiki, kuzitunza na ameahidi wao kama vionhozi watazisimamia pikipiki hizo na kuhakikisha zinafanya kazi iliyokusudiwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu, Ezekiel H. Magehema ametoa pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania jwa kutoa pikipiki 49 kwa wilaya ya Kyela, ambapo pikipiki 40 zitagawiwa kwa maafisa ugani na 9 kwa watendaji wa kata.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu Ezekiel H. Magehema akitoa taarifa za ugawaji wa pikipiki kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa
Amesema pikipiki hizo zinakwenda kusaidia katika ufanisi wa kazi hasa katika eneo la kilimo na eneo la ukusanyaji wa mapato, pamoja na hayo amesema pikipiki zilizogawiwa kwa watendaji kata zimezingatia ukubwa wa kata, umbali na ufanisi wa kata katika kukusanya mapato.
Mwisho maafisa ugani na watendaji wa kata wamempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuahidi kuongeza ufanisi wa kazi na kuto muangasha katika suala zima la kilimo na uongezaji wa mapato na kuleta maendeleo yenye tija kwa wananchi.
Afisa ugani wa kata ya Kajunjumele ndugu Everisto Mkwele akitoa shukrani zake za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya wenzake mara baada ya kupokea pikpiki.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa