
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera ameongoza kikao cha upotevu wa kokoa zilizohifadhiwa katika ghala la Kyela, kampuni ya Golden traders kilochofanyika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 19/7/2024.
Kikao hicho kimehudhuriwa na kamati ya Ulinzi na Usalama ngazi ya mkoa na wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri,wataalamu mbalimbali ngazi ya wilaya na mkoa pamoja na wadau wa kokoa kampuni ya Mohamed enterprises, Golden traders.
Katika kikao hicho Mhe. Mkuu wa Mkoa amebaini upotevu wa gunia 252, za kokoa zenye thamani ya Tsh. milioni 441 zilizohifadhiwa ghala la Kyela mjini, linalomilikiwa na kampuni ya Golden trader kupitia mashindano ya mnada wa 3 uliofanyika tarehe 15/7/2024.
Aidhaa Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa suluhu juu ya tukio hilo kupitia tamko la Mhe. Waziri wa kilimo Hussein Bashe, ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria na kufanya uchunguzi wa kina kwa viongozi juu ya miamala iliyotumika kwa wakati huo. Ameiagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi.
Vilevile Mhe. Mkuu wa Mkoa ameiagiza kampuni ya Golden trader kupatikana kwa fedha hiyo ndani ya siku ya saba kuanzia tarehe 19/7/2024 na kutoa taarifa ofisi ya Mhe. Mkuu wa wilaya pindi fedha hiyo itakapopatikana.
Pia Mhe. Mkuu wa mkoa amewataka Golden trader kusimamisha taratibu za zabuni ya kokoa mpaka pale watakaporidhia kutoa ruhusa kwa mara nyingine.
Aidhaa Mhe. Mkuu wa mkoa ameomba kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kyela kwa kushirikiana na kamati ya Usalama ngazi ya mkoa kuendelea kusaidia uimarishaji wa ushirika ndani ya wilaya ili kusaidia wananchi hususani wakulima kupata stahiki zao.
Kwa upande wake Mhe. Mkuu wa wilaya Josephine Manase ameipongeza kampuni ya Mahamed enterprises ikiwemo mnunuzi wa kokoa wa kampuni hiyo kwa ukaguzi na usimamizi mzuri wa kampuni yao kuweza kubaini tatizo hilo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa