Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera amekamilisha ziara yake ya siku 3 wilayani Kyela tarehe 11/10/2023.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amekagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Ibanda kata ya Ibanda, mradi wa ujenzi wa shule mpya ya wasichana ya mkoa inayojengwa katika kata ya Busale pia amekagua mradi wa maji lema katika kata ya Busale.
Akikamilisha ziara yake ya siku 3 wilayani Kyela, Mhe. Mkuu wa Mkoa ameagiza majengo ya shule mpya ya Sekondari Ibanda kumalizika kwa wakati ili wanafunzi waanze kusoma katika shule hiyo.
Amewataka viongozi kusimamia mradi wa shule ya Ibanda na amesema kufikia tarehe 11/11/2023 shule ifunguliwe.
Amemtaka Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase akishirikiana na Mhe. Mbunge wajimbo la Kyela Ally Mlaghila Jumbe pamoja na ofisi ya TARURA, kukaa na mkandarasi anaetengeneza barabara ya junction Kiwira Port, kusaidia kuchonga barabara hadi katika shule mpya ya sekondari Ibanda.
Hata hivyo Mhe. Mkuu wa mkoa ametoa maagizo ya kusimamia miradi ya maendeleo usiku na mchana ikiwemo usimamizi wa shule mpya ya wasichana ya mkoa inayojengwa katika kata ya Busale ili iweze kukamilika kwa wakati.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Josephine Manase, ametoa shukrani zake za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuletea fedha ambazo zinasaidia katika utekelezaji wa miradi wilayani Kyela.
Pamoja na shukrani hizo Mhe. Mkuu wa wilaya ameyapokea maagizo yote aliyoyaangiza Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera na kuahidi kuyafanyia kazi kwa wakati.
Awali Mbunge wa jimbo la Kyela Mhe. Ally Mlaghila Jumbe ametoa shukrani kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha ambazo zinawezesha utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali zikiwemo shule za sekondari na msingi.
Pia ameomba ulinzi na utunzaji mzuri wa vifaa vinavyonunuliwa kwaajili ya ujenzi, ili kuyafanya majengo yetu kukamilika yakiwa imara na yenye ubora.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. kingamkono, ametoa pongezi kwa mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Na amemuahidi Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwamba, atashirikiana na viongozi wengine wa wilaya katika kusimamia miradi yote na kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.
Mwisho Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela, Bi. Florah A. Luhala amepokea maagizo yote yaliyotolewa na Mhe. Mkuu wa mkoa na kuahidi kuyatekeleza kwa wakati.
Mwisho
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa