Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Claudia U. Kitta amefanya mkutano na wananchi wa kijiji cha matema, kata ya Matema leo tarehe 21/10/2019, katika viwanja vya ofisi ya kata hiyo.
lengo la kufanya mkutanao huo ni kutaka kuwasikiliza wananchi kero zao, Katika mkutano huo, Mkuu wa wilaya aliwasikiliza wananchi hao ambao walihitaji kufahamu matumizi ya fedha za michango yao.
Aidha wananchi walitoa kero zao, ambazo zilimtaka mtendaji wa kata hiyo ndugu Edsoni Rugalabama, kutoa ufafanuzi wa matumizi ya fedha shilingi milioni 4,190,000/=, ambazo zilichangwa na wananchi hao.
Akitoa maelezo juu ya pesa hizo, mtendaji huyo alionekana kutokuwa na maelezo mazuri, ambayo yalimpekea kutoaminika na viongozi pamoja na wananchi wake.
Hata hivyo ndugu Edson Rugalabama, amekili kukaa na pesa zaidi ya miezi 6, kiasi cha shilingi milioni 1,740,000/=, ambazo ni tozo za faini mbalimbali zinazotozwa na mtendaji huyo kutoka kwa wananchi kwa makosa tofauti tofauti.
Kwa upande wake mtendaji wa kijiji hicho ndugu Neson Mwafingulu, alitoa ufafanuzi wa jinsi alivyokuwa akiwasiliana na mtendaji wa kata, ili aje kutoa ufanunuzi wa taarifa ya matumizi ya shilingi 4,190,000/=, na bakaa ya shilingi 1,44,000/= Na matumizi hayo hayakuwa na ushirikishwaji wa aina yoyote wala kuwa na ufafanuzi wa matumizi ya pesa hizo.
Hata hivyo jitihada zake ziligonga mwamba, na taarifa hiyo haikuweza kufikishwa kwa wananchi kwa muda walioitaka taarifa hiyo, na kuamua kufikisha kero yao kwa Mkuu wa wilaya ya Kyela.
Baada ya wananchi kutoa kero zao, Mkuu wa wilaya ya Kyela aliwatuliza wananchi hao, waliokuwa na hasira kubwa, na kutoa maamuzi ya kumchukua mtendaji wa kijiji hicho ndugu Nason Mwafingulu, pamoja na mtendaji wa kata hiyo ndugu Edson Rugalabama na kuwafikisha katika kituo cha polisi, kwa maelezo zaidi.
Mwisho Mkuu wa wilaya aliagiza wakaguzi kwenda katika kata hiyo, na kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha hizo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa