Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase ameendelea na ziara yakusikiliza na kutatua kero za wananchi Wilayani Kyela ambapo tarehe 04.07.2024, ametembelea kata ya Lusungo kijiji cha Lukama, kwa lengo lakusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Mhe. Josephine Manase amefanikiwa kutatua kero mbalimbali katika kijiji cha Lukama ikiwemo kero ya upatikanaji wa umeme Pamoja na ukosefu wa Mtendaji wa kijiji, ambapo hapo awali hapakuwa na Mtendaji katika kijiji hicho.
Kuhusu suala la umeme, Mratibu wa "REA" wilaya ya Kyela Ndugu. Jairo Simion Sichura amesema kuwa kijiji cha Lukama kata Lusungo kipo katika mpango wa kuwekewa umeme, na wapo katika hatua ya kumtafuta mkandarasi wa kafanya shughuli hiyo, mara atakapo patikana atatambulishwa katika kijiji na ataanza kazi ya kuwawekea umeme wanakijiji wa Lukama.
Aidha suala la kukosekana kwa mtendaji wa kijiji katika kijiji hicho Mhe. Josephine Manase Mkuu wa wilaya ya Kyela alimtaka Afisa Utumishi wilaya atolee ufafanuzi jambo hilo, ambapo Ndugu. Michael Celestine Tolage amesema; suala hilo litakamilika baada ya wiki 2, Mtendajibwa kijiji atakuwa amepatikana.
Vilevile kuhusu suala la Elimu, ambapo wanakijiji wa Lukama walitoa malalamiko kuhusu uhaba wa walimu, ambapo Kaimu Afisa Elimu msingi Ndugu, Kanzale Mwangungulu alilitolea ufafanuzi kwa kusema, kuwa pindi Serikali ikitoa ajira za Walimu basi shule ya msingi Lukama itapewa kipaumbele cha kuletewa walimu.
Hata hivyo katika kutilia Mkazo Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amewaambia Wananchi wa Kata ya Lusungo kwa wale wote wenye watoto wao ambao wamesomea kada ya Ualimu wajitolee kwa Muda, katika shule hiyo mpaka pale serikali itakapo toa ajira za walimu.
Akijibu swali la mwanakijiji kuhusu kukithiri kwa mimba za utotoni katika kijiji hicho Mhe. Josephine Manase amesema Ni kosa kubwa kwa mtu kumpa mimba mwanafunzi, aidha Mhe. Manase ameendelea kutoa onyo kali kwa mtu yeyote atakae patikana na hatia hiyo, hatua kali za kisheria zitachuliwa, Hivyo amewataka wananchi hao kushirikiana ili kupiga vita mimba za utotoni.
Pamoja na hayo, Mhe. Mkuu wa wilaya amewataka wananchi waliopata maji majumbani kwao kuyalipia maji hayo, ili kuiwezesha wizara husika kuwafikia watu wengi katika kusambaza huduma ya maji, pia kurekebisha miundo mbinu ya maji pale inapohitajika.
Pamoja nakusikiliza kero za wananchi wa kata ya Lusungo Mhe. Josephine Manase ameendelea kuhamasisha wananchi kuendelea kuilinda na kuitunza amani tuliyonayo Watanzania kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa