Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amefanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Ngana tarehe 30/05/2024.
Katika ziara yake, Mhe. Mkuu wa wilaya, ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri Bi. Florah Luhala akiwa na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo, pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za serikali.
Akizungumza na wakazi wa kata hiyo, Mhe. Josephine Manase, ameitaka kamati ya maendeleo kata ya Ngana kusimamia matumizi mazuri ya fedha, ili kukamilisha miradi mbalimbali iliyopo katika kata ya Ngana, pia amewaomba wananchi kuendeleza ushirikiano wao na serikali ili kuhakikisha shughuli za maendeleo zinafanyika na kukamilika kwa wakati.
Akijibu kero, ikiwa ni pamoja na Wananchi kutosomewa mapato na matumizi, ubovu wa miundombinu kwa baadhi ya maeneo, ushuru kwa wakulima, Mhe. Josephine amesema;
Kero hizo zinafanyiwa kazi na kuomba wananchi kuwa wavumilivu, kwani kuna baadhi ya kero zitatatuliwa na serikali mara baada ya kupita kwa msimu wa mvua ikiwemo kero ya daraja katika kijiji cha ushirika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Bi. Florah A. Luhala, ameahidi kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili wananchi hao, ikiwemo ujenzi wa choo soko la Kasumulu, Suala la maji katika shule ya msingi Kasumulu, na kuwaomba wananchi kuwa na uangalizi mzuri wa fedha za miradi zinazotolewa na serikali.
Sambamba na hayo Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Kyela, amemaliza kwa kuwaomba wananchi kutunza mazingira ili kuepukana na hali ya jangwa, kupitia athari za ukataji wa miti hovyo ikiwa ni kuendeleza jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, anaetutaka tutunze mazingira kila siku na kuzingatia matumizi ya nishati Safi.
Mwisho...........
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa