Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani Kyela, tarehe 26/06/2024.
Akiwa katika ziara yake, Mhe. Mkuu wa wilaya amemsisitiza mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi ikiwemo na upatikanaji wa hati ya maeneo ya miradi hasa mradi wa nyumba ya Mkurugenzi na mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri katika kata ya Bondeni.
Aidha amewataka viongozi kuwa makini katika matumizi ya fedha za miradi ili kuhakikisha miradi inakamilika na huduma zinaanza kutolewa kwa wakati, ameyasema haya akiwa katika ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa shule ya Kokoa Girls inayojengwa katika kata ya Nkokwa hapa wilayani Kyela.
Pia amewapongeza wanakamati wanaosimamia ujenzi kwa kuendelea kusimamia mradi, kwani baada ya kukamilika kwa mradi, utakuwa faida kwa wananchi wa kata ya Nkokwa na Nchi yetu kwa ujumla wake.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa