Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Josephine Manase ameongoza kikao cha baraza la biashara katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 12.2.2025.
Miongoni mwa waliohudhuria baraza Hilo ni pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama, wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi,pamoja na wafanyabiashara wa wilaya ya Kyela.
Akizungumza na wajumbe kwenye baraza hilo Mhe.Mkuu wa Wilaya ameomba ofisi ya Mkurugenzi kutenga bajeti maalumu kwa ajili ya kununua eneo litakalotumika kujenga soko la Halmashauri la kisasa.
Pia Mhe.Mkuu wa Wilaya ameitaka Halmashauri kujenga ushirikiano mzuri na wafanyabiashara ndani ya Wilaya ya Kyela ili kuhakikisha sekta ya biashara inakua.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa