Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase, ameongoza kikao cha tathmini ya mkataba wa lishe ngazi ya wilaya leo tarehe 31/07/2024, katika ukumbi wa Hospitali ya wilaya.
Akiwa katika kikao hicho Mhe. Mkuu wa wilaya amewapongeza watendaji kwa kuendelea kutoa hamasa ya lishe kwenye kata zao, na amewataka watendaji waige kwa wengine ambao wanafanya vizuri katika suala la lishe ili kutokomeza hali duni ya lishe katika wilaya yetu.
Aidha amesema kwa sasa suala la lishe wilayani Kyela inaendelea vizuri, na tutaendelea na kampeni ya lishe sababu kampeni hii ni kwa Taifa zima.
Amesema, kwa mtendaji yeyote atakaefanya vizuri siku ya lishe, na atakaetoa rangi nyekundu katika "score card" atatoa zawadi kwa watendaji 3 ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji.
Aidha Mhe. Mkuu wa wilaya amesema ni lazima tushirikiane kwa pamoja kuimba kampeni ya lishe, ili kumuunga mkono Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kuzakisha kizazi bora katika nchi yetu.
Pamomja na hayo Mhe. Mkuu wa wilaya amewakumbusha walimu kutumia mashamba ya shule kama yapo kulima mazao ya chakula, yatakayowasaidia wanafunzi kupata chakula na si vinginevyo.
Pia amewataka watendaji wa kata na vijiji, kuendelea kutunza amani iliyopo katika kuelekea zoezi la uchaguzi, amesema, kila mtendaji wa kata ajue takwimu ya watu wake katika eneo lake ili kuondoa mamluki katika zoezi zima la uchaguzi.
Awali Afisa lishe (W), ndugu Allen Mutalemwa Binamungu, alitambulisha wiki ya unyonyeshaji duniani, kwa wajumbe wa kikao. Ambayo ni tarehe 1-7 Agosti 2024. Na kauli mbiu katika wiki ya unyonyeshaji ni "ZIBA PENGO, WEZESHA UNYONYESHAJI KWA WOTE".
Aliongeza kwa kutaja faida za kuwanyonyesha watoto maziwa ya mama na mbinu za kuhakikisha watoto wananyonyeshwa maziwa ya mama bila vikwazo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa