Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase (mbele) akiongoza msafara kuelekea eneo ambapo shule ya wasichana ya Mkoa itajengwa.
Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase leo juni 28, 2023, ametembelea eneo la kata ya Busale wilayani Kyela, ambapo mradi wa shule ya wasichana ya mkoa inatarajiwa kuanza kujengwa.
Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, wakuu wa taasisi, Idara na vitengo.
Akizungumza katika eneo la mradi, Mhe. Mkuu wa wilaya amesema, anatoa shukrani zake za dhati kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae ameikumbuka wilaya ya Kyela na kutuletea mradi wa shilingi bilioni 4 ambapo hadi muda huu shilingi bilioni 3 tayari zipo katika akaunti tayari kwa kuanza mradi wa shule ya wasichana ya mkoa. Pia ameahidi kuto muangusha Mhe. Rais kwa kuusimamia mradi na kuukamilisha kwa wakati.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa wilaya amewataka wataalam kuhakikisha miundombinu ya barabara inafika kwa urahisi katika eneo la mradi ikiwemo, huduma za maji na umeme ili kuukamilisha mradi kwa mda usiozidi miezi 6.
"Naomba miundo mbinu ya barabara, umeme na maji isogezwe kwa haraka katika eneo la mradi kwani fedha tunazo na tupo nyuma ya mda" amesema Mhe. Mkuu wa wilaya.
Hata hivyo amemuomba diwani wa kata ya Busale Mhe. Adam Kabeta kuwahamasisha wananchi wa kata yake, kujitokeza kwa wingi kusaidia shughuli ndogondogo katika mradi, ili kuungana na kutambua kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa naendeleo ya wanaKyela.
Hapa ni sehemu ya kata ya Busale wilayani Kyela ambapo mradi wa shule ya wasichana ya mkoa inatarajiwa kuanza kujengwa
Aidha amesema, ushirikiano baina ya wananchi uimarishwe ili kuwe na ulinzi shirikishi katika vifaa vya ujenzi wa mradi.
Mwisho Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ameweza kutembelea mradi wa maji Lema ili kujiridhisha na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.
Hapa ni eneo la tenki la mradi wa maji Lema uliopo kata ya Busale.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa