Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe Josephine Manase amekagua miradi ya maendeleo Kijiji cha Ndwanga na Kijiji cha Katumba katika Kata ya Katumba Songwe tarehe 22.7.2025.
Miradi iliyokaguliwa ni Nyumba ya Afisa Ugani inayogharimu Tsh.Milioni 40.
Mradi wa Wash katika Zahanati ya Katumbasongwe unaojumuisha matundu 5 ya vyoo, kinawia mikono, upanuzi wa chumba cha Wazazi wanaojufungua na ujenzi wa kichomea taka, katika ujenzi huu Serikali imetoa Tsh.milioni 43 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi huo.
Mhe.Mkuu wa Wilaya ameupongeza uongozi wa Kata na Uongozi wa Kijiji kwa ushirikiano mzuri wa usimamizi wa Miradi hiyo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa