Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amefanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi kata ya Ipyana na kata ya Ikolo tarehe 27/06/2024.
Katika ziara yake Mhe. Mkuu wa wilaya ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri Dkt. Saumu Kumbisaga, wakuu wa Idara na Vitengo, pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali.
Aidhaa Mhe. Mkuu wa wilaya ameishukuru serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha zinazosaidia kuanzisha na kuboresha miradi mbalimbali katika wilaya ya Kyela.
Baadhi ya kero zilizosikilizwa ni pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari kata ya Ipyana, pamoja na changamoto ya ushuru kwa wakulima wadogo wa mpunga kata ya Ikolo.
Kwa upande wa kero ya ushuru kwa wakulima wa mpunga, Mhe. Mkuu wa wilaya amewataka wakulima kuchukua vibali kutoka kwa watendaji wa kata, vitakavyowasaidia kusafirisha mazao yao kutoka shambani bila usumbufu.
Pia amewaomba viongozi wa kata ya Ipyana kufanya vikao na wananchi ili waweze kutoa taarifa za mapato na matumizi ya michango inayotolewa na wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya miradi.
Aidhaa Mhe. Mkuu wa wilaya, amemaliza kwa kuwaomba viongozi wa kata hizo ikiwemo Wahe. Madiwani na Wenyekiti wa vitongoji kuondoa migogoro ya kisiasa baina yao, hasa tunapo elekea katika kipindi hiki cha uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa.
Aidha amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuhakiki taarifa zao katika daftari la kudumu la mpiga kura ili kuepusha usumbufu wakati wa uchaguzi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa