Akijibu kero za wanananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Makwale tarehe 18/05/2023, Mkuu wa wilaya ya Kyela, Mheshimiwa Josephine K. Manase amesema,
Wananchi wa kata ya Makwale wanapaswa kupendana na kuacha kugombana wao kwa wao, hasa katika makanisa, ambapo viongozi wa dini mbalimbali katani humo, ndiyo wamekuwa vinara kwa kugombana.
Aliwataka viongozi wa dini kukaa na kumaliza tofauti zao, kwa kufanya hivyo waumini na wananchi wataishi kwa amani katika kata yao.
"Ninaamini siku mkiniita wanaMakwale, mtaniita mkiwa mmeitafuta amani, naomba tupendane na mimi nitawaunga mkono katika maendeleo hatua kwa hatua". amesema Mhe. Manase.
Aidha amemshukuru Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaona wakulima wa Makwale, kwa kuongeza vituo vya usamabaji wa Mbolea. Aidha amesema anaamini ipo siku kata ya Makwale kituo cha usambazaji wa pembejeo kitapatikana.
Kuhusiana na suala la umeme, Mhe. Mkuu wa wilaya amesema, wao kama viongozi wameendelea kuwasemea wananchi ambao hawajapata umeme, na amesema wananchi hao wawe wavumilivu ili kusubiri Mpango wa umeme wa REA katika awamu nyingine ya usamabazaji wa umeme unaokuja. Hivyo kila mwananchi atapata huduma ya umeme.
Pamoja na hayo Mhe. Manase amesema ukarabati wa ofisi ya mahakama kuna mradi utakao tekelezwa kuanzia mwezi wa 6 na Mahakama itaanza kujengwa.
Aidha amewaonya wakinamama wanaokopeshana, kuwa na katiba nzuri katika vikundi vyao vya kukopeshana alimaarufu "Kausha Damu" Pia amewataka kuacha kukopa katika vikundi hivyo ikiwa hawana uwezo wa kulipa mikopo, ili kuondoa tatizo la migogoro katika familia zao.
Hata hivyo Mhe Mkuu wa wilaya, amewataka wananchi kukubaliana viwango vya michango ya maendeleo kutokana na hali za wananchi ili kila mwananchi aweze kuchangia bila kuumizwa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa