• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mkuu Wa Wilaya Ya Kyela Awataka Wananchi Kata Ya Makwale Kuishi Kwa Upendo

Imewekwa Kwenye: May 19th, 2023

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Makwale tarehe 18/05/2023, Mkuu wa wilaya ya Mheshimiwa Josephine K. Manase amesema,

Wananchi wa kata ya Makwale wanapaswa kupendana na kuacha kugombana wao kwa wao, hasa katika makanisa,  ambapo viongozi wa dini mbalimbali katani humo, ndiyo wamekuwa vinara kwa kugombana.
Aliwataka viongozi wa dini kukaa na kumaliza tofauti zao, kwa kufanya hivyo waumini na wananchi wataishi kwa amani katika kata yao.

"Ninaamini siku mkiniita wanaMakwale, mtaniita mkiwa mmeitafuta amani, naomba tupendane na mimi nitawaunga mkono katika maendeleo hatua kwa hatua". amesema Mhe. Manase.

Aidha amemshukuru Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaona wakulima wa Makwale, kwa kuongeza vituo vya usamabaji wa Mbolea ambapo hadi sasa kuna kituo kata ya Matema na Mababu kata ambazo ni jirani na kata ya Makwale. Aidha amesema anaamini ipo siku kata ya Makwale kituo cha usambazaji wa pembejeo kitapatikana.

Kuhusiana na suala la umeme, Mhe. Mkuu wa wilaya amesema, wao kama viongozi wameendelea kuwasemea wananchi ambao hawajapata umeme, na amesema wananchi hao wawe wavumilivu ili kusubiri Mpango mpya wa usambazaji wa umeme wa REA. Amewahakikishia wananchi wa Makwale kuwa, kila mwananchi atapata huduma ya umeme.

Pamoja na hayo Mhe. Manase amesema ujenzi wa ofisi ya mahakama upo njiani, kuanzia mwezi wa 6 jengo la mahakama mpya katika kata hiyo utaanza.

Ameongeza kwa kusema, Mahakama itaanza kujengwa, Lakini kuhusiana na ukarabati wa ujenzi wa ofisi ya kata Mhe. Mkuu wa wilaya amemtaka Mtendaji kata kulisimamia hilo na kufanya ukarabati wa ofisi ya kata.
Aidha amewaonya wakinamama wanaokopeshana, kuwa na katiba nzuri katika vikundi vyao vya kukopeshana alimaarufu "Kausha Damu" Pia amewataka kuacha kukopa katika vikundi hivyo ikiwa hawana uwezo wa kulipa mikopo, ili kuondoa tatizo la migogoro katika familia zao.

Kuhusiana na michango ya maendeleo kutoka katika jamii, Mhe Mkuu wa wilaya, amewataka wananchi kukubaliana viwango vya michango ya maendeleo kutokana na hali za wananchi ili kila mwananchi aweze kuchangia bila kuumizwa.

Wananchi wa kata ya Makwale wamefurahishwa na ziara ya Mkuu wa wilaya Mhe. Josephine Manase na wamemuomba awe anawatemblea kila wakati ili waweze kutoa kero zao kama walivyofanya katika mkutano huo.

Mwisho.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WALIMU WAKUU,WALIMU WA MANUNUZI, WAKUU WA SHULE,WATENDAJI WA KATA NA WA VIJIJI WAPIGWA MSASA MFUMO WA MANUNUZI (NEST)

    April 24, 2025
  • DED KYELA AFANYA KIKAO NA WATENDAJI KATA CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA UTENDAJI KAZI NA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA

    April 10, 2025
  • DC KYELA AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KUANZIA JULAI HADI DESEMBA 2024

    March 29, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAPONGEZA USIMAMIZI MZURI WA MRADI WA JENGO LA MAMA NA MTOTO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA

    March 20, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa