Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Mheshimiwa Ismail Mlawa, amewatoa hofu wakulima wa wilayani Kyela juu ya wanyama waharibifu wa mazao (Ngedere) ambao wamekuwa ni kikwazo katika mazao ya kilimo wilayani hapa.
Mheshimiwa Ismail Mlawa ameyasema haya katika kikao cha baraza la Waheshimiwa Madiwani la robo ya 4 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri tarehe 30/08/2022.
Amesema hadi sasa risasi maalum za kufukuzia ngedere tayari zimekwisha nunuliwa na kwamba kinachosubiriwa ni utelezaji wa zoezi la kuwaondoa ngedere kwenye mashamba.
Aidha alisema, wananchi wanatakiwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika na sio kuchukua sheria mkononi kwa kuwaua.
Akizungumzia suala la uandikishwaji wa pembejeo kwa wakulima alisema, zoezi hilo linaendelea na anauhakika kuwa zoezi litaendelea kama kawaida na kwamba wakulima wote watafikiwa.
Alifafanua kuwa wakulima watakaoandikishwa ni wale wenye mashamba na wanaofanya shughuli za kilimo wilayani Kyela na kwamba mkulima yeyote mwenye shamba nje ya wilaya, atalazimika kujiandikisha eneo lilipo shamba lake.
“Sensa ya watu na makazi imesababisha uandikishwaji wa wanufaika wa pembejeo kusuasua lakini baada ya zoezi la sensa kukamilika zoezi litaendelea na kuwafikia wakulima wote, lakini naomba nitoe ufafanuzi kwamba wakulima watakaondikishwa ni wale wote ambao wana mashamba hapa wilayani Kyela tu hivyo kama mashamba yako yapo nje ya wilaya hii utajiandikisha yaliko,” alisema Mlawa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Katule Kingamkono alisema kila mkulima mwenye kigezo atapata pembejeo za kilimo.
Aliwaomba wataribu wa zoezi hilo kuwa waaminifu kwa kuhakikisha kila mkulima anayestahili apewe mbolea kwa bei elekezi ya serikali na kumuwezesha kupata mavuno mengi.
Mwisho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa