Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase akimpa mtoto chanjo ya Polio katika zoezi la ufunguzi wa kampeni ya chanjo katika eneo la kitongoji cha Roma wilayani Kyela.
Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Josephine Manase tarehe 21/09/2023 amezindua kampeni ya utoaji wa chanjo ya Polio, zoezi limefanyika katika kata ya Mbugani kitongoji cha Roma.
Zoezi limehudhuriwa na Mbunge wa jimbo la Kyela Mhe. Ally Mlaghila Jumbe, Wawakilishi kutoka wizara ya Afya na Mkoa, Katibu tawala wa wilaya Ndugu. Sabrina H. Ruhwey, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Ndugu Frolah A. Luhala, Mkuu wa Idara ya Afya, Ustawi wa jamii na Lishe wa wilaya Dr. Saumu Kumbisaga pamoja na timu za utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio hapa wilayani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya chanjo, Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amesema;
Lengo la Serikali la kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio, ni kumkinga mtoto dhidi ya ugonjwa hatari wa Polio, ugonjwa ambao hauna dawa.
Amesema kampeni inawahusu watoto wote walio chini ya miaka 8, ili kuwakinga na maambukizi ya ugonjwa wa Polio ambao ukimpata mtoto anaweza akapata ulemavu wa kudumu au unaweza kumsababishia kifo.
Aidha amewataka wazazi, walezi kuwatoa watoto wao ili waweze kupata chanjo katika kampeni hizi zilizoanza tarehe 21-24/09/2023 ili kumitiza malengo ya idadi ya watoto ambao Serikali imeazimia kuwafikia katika wilaya ya Kyela.
Nae Mbunge wa jimbo la Kyela Mhe. Ally Mlaghila Jumbe ametoa pongezi za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali watoto wa Tanzania, kwani watoto ndio Taifa la baadae.
"Wazazi tukumbuke kuwa watoto hawa ndio Taifa la baadae hivyo tusipowapa chanjo leo, tunatengeneza Taifa dhaifu' amesema Mhe. Ally.
Mwisho amewata wazazi kujitokeza kuwachanja watoto wao kwani zoezi hili linafanyika kwa kufuata nyumba kwa nyumba, hivyo uhakika wa kupata chanjo kwa kila mtoto upo, kinacho hitajika ni ushirikiano baina ya wazazi na walezi wa watoto waliopo majumbani mwetu.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa