Licha ya kuzunguka kila kata ili kuwafuata wananchi na kusikiliza kero, Leo tarehe 20/03/2024, Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase ameandaa, kikao katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri na kusikiliza kero za wananchi, kikao kilichorushwa mubashara kupitia redio yetu ya jamii Keifo FM, na wananchi wote wamepata fulsa ya kusikiliza utatuzi wa kero zao.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu tawala wa wilaya Bi. Sabrina Hamoud, Kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bi. Lidya Herbert, wakuu wa Idara na vitengo wa halmashauri, wakuu wa Taasisi za Serikali, pamoja na wanachi wenye kero binafsi na za jumuia.
Katika kikao hicho Mhe. Mkuu wa wilaya amewashukuru watumishi na wanachi waliojitokeza pia ametumia nafasi hiyo kuwakimbusha wananchi kuishi kwa amani, pamoja na kuilinda wilaya yetu dhidi ya wahamiaji haramu.
Amewataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo husika pale wanapokuwa na mashaka na mtu yeyote ambae ni mgeni katika kijiji au kata, ili kujua uraia wake, kwani wilaya yetu ipo mpakani, hivyo ni kwa baadhi ya wageni kuingia bila kufuata taratibu za uhamiaji na baadae kuwa tatizo kwa jamii ya wanaKyela na Taifa kwa ujumla.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa