Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine K. Manase amezindua vyumba 4 vya madarasa vyenye thamani ya shilingi 80,000,000/= katika shule ya sekondari Njisi iliyopo kata ya Njisi hapa wilayani Kyela 25/04/2023.
Uzinduzi huo umefanyika ikiwa ni utekelezaji wa moja ya shughuli za maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar.
Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa madarasa hayo, Mheshimiwa Mkuu wa wilaya amesema, katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa nchi yetu ya Tanzania, tunapaswa kuwashukuru waasisi wa Muungano wetu, na kutufanya wananchi kuwa huru hadi leo hii, pia nchi yetu imekuwa na amani kwa sababu ya umoja wetu.
"Umoja wetu ndiyo Muungano wetu, maana yake bila huu umoja hakauna Muungano" amesema Mhe. Manase.
Aidha amewaomba wananchi kumuunga mkono Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii katika maadhimisho haya ya miaka 59 ya Muungano wetu.
Ameongeza kwa kusema Mhe. Rais wetu ametufanyia mengi wanaKyela ikiwemo uanzishaji wa miradi ya maendeleo kila kona ya wilaya yetu.
Katika kuadhimisha sherehe za miaka 59 ya Muungano wa nchi yetu, halmashauri ya wilaya kwa kushirikiana na wananchi, imeweza kutekeleza shughuli mbalimbali katika jamii ikiwemo,
Shughuli za upandaji wa miti, ikiwa hadi kufikia tarehe 25/04/2023 miti 61,000 imepandwa katika mazingira tofauti tofauti ndani ya wilaya yetu. Pamoja na hayo shughuli za usafi wa mazingira zimefanyika pia uandaaji wa makala fupifupi ambazo zimewashirikisha wazee kutoka kwenye jamii zetu, na kupata fulsa ya kuuzungumzia umuhimu wa Muungano wetu.
Mwisho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa