Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase azindua rasmi kampeni ya utoaji wa chanjo ya surua na lubela kwa watoto wote walio chini ya umri wa miaka 5, leo tarehe 15.02.2024 katika kata ya Ndandalo wilayani Kyela.
Akizindua kampeni Hiyo Mhe. Manase amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi, kuwaleta watoto wao kupata chanjo ya ugonjwa wa surua ili kuepuka athari zinazotokana na ugonjwa wa surua, ambapo chanjo itatolewa kuanzia tarehe 15.02.2024 mpaka tarehe 18.02.2024.
Aidha Mhe. Mkuu wa wilaya ya Kyela amewapongeza wananchi waliojitokeza siku ya leo kwa kuwaleta watoto wao kwaajili ya kupatiwa chanjo ya ugonjwa wa surua na kuwataka kuwa mabalozi kwa wananchi wenzao.
Pamoja na hayo Mhe. Manase amewaomba wananchi, kuepukana na imani potofu juu ya ugonjwa wa surua na lubela. Amethibisha kwamba, chanjo zinazotolewa, zimethibishwa ubora na wataalamu wa afya wote ulimwenguni na ni salama kwa matumizi ya Mwanadamu hasa watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Mwisho Mhe. Mkuu wa wilaya ya Kyela ametoa faida mbalimbali zitokanazo na chanjo hiyo ya ugonjwa wa Surua na lubela, ikiwemo kumkinga mtoto dhidi ya uoni hafifu au upofu ikiwa ni madhara yatokanayo na ugonjwa wa surua.
Aidha chanjo ya surua inamkinga mtoto na vifo visivyo vya lazima.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa