Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amezindua zoezi la ugawaji wa miche ya miti ipatayo 20088, kwa wakulima na baadhi ya taasisi, ikiwemo miche 15,666 ya michikichi na miche 4,422 ya kakao.
Akizindua ugawaji wa miche hiyo leo tarehe 14.02.2024 Mhe. Manase amewataka wakulima kuhakikisha miche hiyo wanaitunza na kuikuza kwa namna nzuri, ili iweze kuleta tija na manufaa katika kuongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja ili kujikwamua na hali kiuchumi.
Aidha Mhe. Josephine Manase, amewataka wataalam wa masuala ya kilimo, kuendelea kutoa elimu jinsi ya kuitunza miche hiyo mpaka kufikia hatua ya kuzalisha mafuta, ikiwa ni pamoja na zao la kakao na kutimiza lengo lililokusudiwa la kuwanufaisha wananchi wa wilaya ya Kyela.
Pamoja na hayo Mhe. Manase amesisitiza kuzalishwa kwa wingi miche hiyo katika Idara husika, ili tuweze kuwasaidia wananchi, kupambana na kukuza uchumi wao.
Mwisho Kaimu Mkuu wa Idara ya Kilimo nduguwila Pantaleo Mushi, amesema ataendelea kuwatuma wataalam, watakao fuatilia kwa ukaribu miche hiyo ili kuhakikisha inakua katika namna nzuri inayo hitajika, na kuleta mafanikio kwa wananchi wilayani Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa