Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amefanya ziara ya kusiliza kero za wananchi katika kata za Mikoroshini na Bondeni tarehe 05/10/2023.
Mheshimiwa Manase katika ziara yake ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Bi. Florah A. Luhala, Katibu Tawala (W) Bi. Sabrina H. Ruhwey, Kamati ya Ulinzi na na Usalama (W), viongozi wa taasisi mbalimbali za serikali pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo.
Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase, amezungumzia suala la barabara na kuwataka, Viongozi wa Serikali katika kata ya Mikoroshini kukaa na wananchi wa kata ya Mikoroshini ili kuwaomba wananchi wote wairuhusu Serikali ibomoe majengo yaliyojengwa katika hifadhi ya barabara ili kupisha ujenzi wa barabara mpya katika kata ya Mikoroshini.
Kuhusiana na suala la Afya Mhe Mkuu wa wilaya ya kyela amesema, kesi za malalamiko ya akina mama wajawazito zimekua nyingi, ameahidi kuzifanyia kazi kwa kukaa na watoa huduma za afya wa hospitali ya wilaya na kutatua kero za akina mama wote.
Pia amesema ataandaa mpango wa kutoa Elimu kwa akina mama kuhusiana na masuala ya uzazi ili akina mama waweze kuwa na uelewa mpana kuhusu masuala ya Afya ya uzazi na kuepuka changamoto ya kutapeliwa na watumishi wenye tabia zisizo za kiungwana.
Pamoja na hayo Mhe. Manase amewaomba wananchi wa kata ya Mikoroshini kushirikiana katika suala la malezi ya watoto wakike ili kuepusha tabia mbovu zinazoweza kuleta madhara katika kata hiyo ikiwemo kuacha shule.
"Mtoto wa mwenzio ni wako hivyo ukimuona mtoto wa mwenzio anaenda mrama basi mrekebishe" amesema Mhe. Manase.
Akiwa katika kata ya Bondeni Mhe. Mkuu wa wilaya, amewataka wananchi wa kata ya Bondeni kukaa na kujadiliana, jinsi ya kupata eneo la kijenga zahanati na waliwasilishe Halmashauri ili walitengee bajeti kwa utekelezaji.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Bi. Florah A Luhala amewataka wananchi wa kata ya Mikoroshini kulipa madeni ya mikopo wanayo kopa katika taasisi zinazojihusisha na kukopesha pesa ili kuepuka changamoto ya kunyang'anywa mali binafsi, ambazo huwekwa rehani na mdaiwa.
Aidha Bi. Florah A. Luhala ameongeza kuwa Wazee wenye uhitaji maalumu waliokosa kunufaika na pesa ya TASAF, amewataka kuomba tena wakiwa na taarifa muhimu ili waweze kushughulikiwa na wataalam.
Mwisho ameahidi kuwa wahanga wote wenye sifa watafaidika na mfuko huo wa TASAF bila upendeleo wowote.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa