Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase, tarehe 16.04.2024 ameendelea na ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa katika wilaya ya Kyela.
Mhe. Manase ametembelea miradi, ikiwemo ujenzi wa matundu 22 ya vyoo katika Shule ya msingi Mbogela, ujenzi wa matundu 11 ya vyoo katika shule ya msingi Kikusya, Mradi wa maji safi katika zahanati ya Kandete,ujenzi wa bwalo la wanafunzi wenye uhitaji maalumu, ujenzi wa jengo la mama na Mtoto katika kituo cha Afya cha Kilasilo,Ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Lubele na Mradi wa shule ya Sekondari ya wasichana ya mkoa inayojengwa kata ya Busale.
Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Kyela amewataka Viongozi ngazi ya kata kutambua Lengo la kuletwa kwa fedha za miradi ya Maendeleo kuwa ni kutatua kero mbalimbali za wanachi.
Aidha amewataka viongozi wa kata, kuwa makini katika usimamizi wa miradi hiyo na kuimaliza kwa wakati uliopangwa ili miradi iweze kutoa huduma katika jamii.
Pamoja na hayo, Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase, amewataka Viongozi na wasimamizi wa miradi Kuitambulisha miradi hiyo kwa wananchi ili kuwaweka bayana kufahamu juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hata hivyo Mhe. Manase amesema hatosita kuwachukulia hatua watu wote wanaokwamisha miradi ya Maendeleo kwani kufanya hivyo nikukwamisha juhudi za Mhe. Rais.
Pia Mhe. Manase ametoa wito kwa Viongozi ngazi ya kata pindi pesa zinaposhuka kwaajili ya utekelezaji wa miradi basi pesa hizo zianze utekelezaji huo maramoja, kwani kuchelewesha utekelezaji ndio sababu ya kukwamisha miradi isimalizike kwa wakati.
Mwisho Mhe. Manase ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushusha fedha katika Wilaya ya Kyela kupitia sekta mbalimbali, pia ametoa shukrani kwa Mbunge wa jimbo la Kyela, Mhe. Ally Jumbe Mlaghila kwakuzidi kuwapambania Wananchi wa Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa