Akizungumza na wananchi wa kata ya Nkuyu na Mababu hapa wilayani Kyela tarehe 08/05/2023, Mhesmiwa Josephine K. Manase amesema,
Ameamua kufanya ziara kwa kila kata ili kusiliza kero za wananchi, kero ambazo zinaweza kuwa ni vikwazo katika kuleta maendeleo.
Mhe. Mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine K. Manase(katikati) akiwa anapokea mifuko 60 ya saruji, mifuko iliyotolewa na Amcos ya "Mali hai" kusaidia ujenzi wa zahanati ya Nkuyu.
Akiwa katika kusikiliza kero za wananchi wa kata ya Mababu, Mhe. Manase amesema amebaini kero kubwa 3 kutoka kwa wananchi wa Mababu, kero hizo ni kama zifuatazo;
Kukosekana kwa umeme, Barabara zisizopitika na wanufaika na Mpango wa TASAF.
Aidha akizungumzia kuhusiana na mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF), Mhe. Mkuu wa wilaya amesema tatizo kubwa ni ukosefu wa elimu kwa wananchi kwani wananchi wamewachagua baadhi ya wanufaika ambao si wahitaji kwa kiwango kikubwa.
Na amewataka wataalam kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kuufahamu mpango huu wa TASAF, na kundoa changamoto hiyo katika jamii.
Kwa upande wa umeme wa REA amesema, Mkataba umesainiwa ikiwa ni phase nyingine ya kusambaza umeme kwenye vitongoji, ambapo Kyela tumepata vitongoji 98, Hivyo amewaagiza viongozi kutoa elimu kwa wananchi wanavyongoja utekelezaji wa mradi huo, ili kuhakikisha kila mmoja anapata huduma ya umeme.
Aidha kwa upande wa kilimo, Mhe. Manase, amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiona kero ya wakulima kufuata "pembejeo" mbolea ya ruzuku kwa umbali mrefu, hivyo katika mwaka wa fedha ujao ameongeza vituo vya kusambaza mbolea ili kumfikia mkulima kwa urahisi zaidi.
Kata ya Mababu na Matema kwa upande wa tarafa ya Ntebela ni mojawapo ya kata ambazo zitakuwa na vituo vya kusambazia pembejeo hizo.
Pamoja na hayo, aliwaomba wananchi wa wilaya ya Kyela, kuulinda ubora wa kokoa, ili kuifanya kuwa na thamani kubwa, amewataka wananchi kutoa taarifa haraka pale wanapomuona mlanguzi analangua wakulima na kuchukua kokoa isiyo na ubora.
Kwa upande wa miundo mbinu amewataka "TARURA" kuendelea kurekebisha barabara zote hasa maeneyo yale ambayo ni muhimu kwa shughuli za wananchi.
Kwa suala la lishe mashuleni, liwe shirikishi ili wazazi wajue juu ya chakula wanachochangia ili kuondoa malalamiko ya wazazi.
Aliendelea kuwaasa wananchi wa Mababu na Kyela kwa ujmla, kuachana na mila kandamizi, hasa zile zinazomuonea mwanamke, mfano mwanamke anafukuzwa katika nyumba mara baada ya mme wake kufariki.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu Ezekiel H. Magehema akiwa kata ya Mababu, amewataka wananchi kuendelea kuchangia chakula cha watoto wao wawapo shuleni, wanafunzi waweze kupata chakula angalau kwa mulo mmoja.
Hata hivyo ndugu Magehema, amewataka wananchi kukabiliana na ngedere, Hata kwa kutumia njia ya asili yaani kuwakamata wachache na kuwavalisha kengele ili wengine wakimbie.
Lakini pia kwa suala la mbwa wanaozagaa, amewataka wananchi kuweka mkakati wa kuwaua mbwa au kuwafungia ndani kampeni inayotakiwa kuanzia ngazi ya ubalozi.
pamoja na hayo amewasisitiza kuwa na vyoo bora, ila serikali ipo kwa ajiri ya kusimamia hayo yote kwa usaidizi wa wananchi.
Mwisho wananchi na viongozi wamepongeza ziara ya Mheshimiwa Mkuu wa wilaya kwa kuwakumbuka katika kusikiliza kero zao. ziara hii ni endelevu kwa kata zote 33 za hapa wilayani Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa