Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase, amefunga mafunzo ya jeshi la akiba tarehe 08/11/2023, katika viwanja vya shule ya sekondari Kiwira Coal Mining "KCM" kata ya Busale, mafunzo yaliyojumisha wahitimu 121, wanawake 20 na wanaume 101.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ametoa pongezi na shukrani kwa viongozi wa kata ya Busale kwa kuhakikisha mafunzo ya ya jeshi la akiba "Mgambo" yameanza na kumalizika salama, Pia amewashukuru Wakufunzi waliohusika kutoa mafunzo na kuwafanya wanafunzi kuhitimu mafunzo hayo kwa viwango vinavyohitajika.
Aidha amewaasa wahitimu wote kutenda matendo mema kwa jamii kama walivyopokea kiapo cha kazi yao.
Amewataka wahitimu wote kuwa mstari wa mbele katika kuilinda, kuwa wazalendo wa nchi yao, Pia amewataka kuwa mstari wa mbele katika kujitolea katika kazi mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
Vilevile amesisitiza uadilifu kwa wahitimu, kwani mafunzo waliyoyapata yakawe ni sehemu ya kupeleka elimu kwa jamii juu ya maadili mema, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na usalama katika kutoa taarifa za uhalifu popote pale unapotokea.
Pamoja na hayo ametoa wito kwa wahitimu kuto yatumia mafunzo katika uhalifu, Hii itaonyesha wahitimu hawakuwa waadilifu na wazalendo katika nchi yao kitendo ambacho Serikali haitafurahishwa na tabia hiyo.
Kuhusiana na ajira, Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ametoa wito kwa makampuni yote ya ulinzi wilayani kuajiri vijana waliopitia katika mafunzo ya Mgambo.
Mheshimiwa Manase amesema, atafurahi sana endapo atawaona wahitimu wanajitokeza katika kusaidia kazi katika miradi ya maendeleo hasa katika mradi wa ujenzi wa shule mpya ya wasichana ya Mkoa katika kata ya Busale.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Bi. Frolah Luhala aliwapongeza wa hitimu wa mafunzo ya Jeshi la akiba na kuwataka kuwa mfano wa kuigwa kwa maadili mema katika jamii.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa