Mkuu wa wilaya ya Kyela (wa pili kutoka kulia) akionyesha kitambulisho cha uraia wakati wa kuzindua zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya Uraia wilayani Kyela.
Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amezindua rasmi zoezi la Ugawaji wa vitambulisho takribani 45,037 vya Uraia wilayani Kyela, zoezi limefanyika katika kata ya Mbugani tarehe 06/12/2023.
Aidha Mhe. Manase amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika kulinda amani kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika kwa watu wenye mashaka nao juu ya Uraia wao, tukizingatia kuwa wilaya ya Kyela ipo mpakani.
Hata hivyo Mhe. Manase amewataka wananchi wa wilaya ya Kyela, kuvitunza vitambulisho hivyo kwa gharama yeyote kwani vina mchango mkubwa katika maisha ya Watanzania.
Vilevile Mhe. Manase amewaomba wakulima wote ambao hawajasajiliwa katika mfumo wa kupata mbolea za ruzuku, wakajisajili kwani vitambulisho vya Uraia sasa vimepatikana, Shukrani kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan, ambae amewarahisishia wakulima kwa kupunguza bei ya mbolea ya ruzuku kwa lengo la kumsaidia mkulima.
Pamoja na hayo Mhe. Manase amewaahidi wakina Mama wote wilaya ya Kyela, kuwa jengo la mama na mtoto linalojengwa katika hospitali ya wilaya litakamilika kwani Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatoa pesa takribani Million 800 kwa lengo la kumalizia jengo hilo ili mara moja lianze kutumika.
Mhe. Manase amehitimisha kwa kuwataka wananchi kuwa wazalendo na kuwaunga mkono viongozi wao katika mambo yote yanayo husu maendeleo ya wilaya.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa