Katika jambo lisilotarajiwa Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Ismail Mlawa, atinga kwa kushtukiza katika viwanja vya Mwakangale hapa wilayani Kyela, ambapo vituo viwili vya redio vya hapa wilayani, redio ya Kyela FM na Keifo FM, kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya, waliandaa tamasha la UVIKO 19. Tamasha lilifanyika tarehe 02/10/2021, likiwa na lengo la kuhamasisha wananchi dhidi ya chanjo ya ugonjwa wa CORONA.
Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Ismail Mlawa(mwenye kofia), akiwa katikati ya wananchi akitazama mpira katika bonanza la UVIKO 19.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Kyela alitumia nafasi hiyo kutoa hamasa kwa wananchi kuchanja chanjo ya UVIKO 19, alisema wananchi wajitokeze kuchanja ili kijilinda na ugonjwa huu hatari ambao umechukua watu wengi duniani, na aliwapongeza waandaji wa Bonanza hilo, kwani lilishirikisha huduma za uchanjaji chanzo hapo hapo uwanjani.
Pia Mheshimiwa Mkuu wa wilaya aliweza kutoa kiasi cha shilingi 200,000/= kwa timu ya Kyela Princes, shilingi 100,000/= kwa timu ya Ngonga Princes ahadi aliyowahadi kuwapa ili kuziendeleza timu hizo za mpira wa miguu kwa wanawake.
Michezo ya Ngoma za asili, mpira wa miguu kwa wanaume na mpira wa miguu kwa wanawake, burudani za mziki zilifanyika pamoja na elimu dhidi ya ugonjwa wa CORONA ilitolewa kupitia Idara ya Afya, yote haya yalifanyika kwa lengo la kutoa hamasa kwa wananchi kuchanja.
Hamasa dhidi ya chanjo ya UVIKO 19, imesaidia sana wananchi wa Kyela kuamka na kuchanja, kwani kila siku idadi ya wananchi kuchanja imekuwa ikiongezeka kwa kasi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa