Msanii Mguli wa mziki hapa Tanzania anaejulikana kwa jina la Mrisho Mpoto na bendi yake, wamemaliza salama kufanya kampeni ya uhamsishaji wa matumizi ya vyoo bora leo tarehe 09//01/2019.
Kampeni hii aliianza tarehe 07/01/2019, na kupata fursa ya kuzunguka kata mbakimbali za Kyela, ikiwemo kata ya Matema, Mababu, Busale, Ipinda na kumalizia Kyela mjini.
Aidha msanii huyo amewataka wananchi wa wilaya ya Kyela, kuachana na utamaduni wa kutokuwa na vyoo bora, kwani wananchi wa Kyela ni wasafi sana, hivyo basi ni aibu kubwa kwao kupendeza wakiwa barabarani ilihali nyumbani hakuna Choo bora.
Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Mhe. Claudia U. Kitta alimhakikishia msanii huyo pamoja na wananchi wa wilaya ya Kyela kuwa, tupo pamoja na serikali ya awamu ya tano, katika kuhakikisha kuwa ifikapo tarehe 30/03/2019, kaya zote nchini kuwa na vyoo bora.
Ila aliomba kwa upande wa wilaya ya Kyela, kukamilisha zoezi hili, ifikapo tarehe 30/06/2019. Sababu kuu ni kutokana na wilaya hii kuwa na maji mengi hivyo basi uchimbaji wa mashimo ya vyoo kuwa mgumu sana kwa kujaa kwa maji mengi katika mashimo hayo bila kufikia malengo.
Pia alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Lucy L. Mganga kwamba, ahakikishe anatafuta takwimu za kaya pamoja na aina za vyoo walivyonavyo, kwani taarifa zilizotolewa na Afisa Afya wa wilaya hazikuwa za kweli.
Mwisho alitoa pongezi kwa serikali ya awamu ya tano kwa kumtumia msanii mlisho mpoto, katika kampeni hizi kwani wananchi wengi wamehamasika, hivyo anaamini kampeni hii inakwenda kutokomeza magonjwa yote ya mlipuko.
Imetolewa na :
Ofisi ya Habari na Mawasiliano
Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa