Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule Kingamkono ameutambulisha mradi mpya wa Serikali wa ujenzi wa shule ya Sekondari yenye Gharama ya Tsh. Milioni 583 katika kata ya Muungano kijiji cha Bukinga tarehe 03/07/2024.
Katika ziara hiyo Mhe. Katule Kingamkono ameambatana na wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali kutoka ofisi ya Mkurugenzi, ikiwemo Afisa Elimu Sekondari, Afisa Manunuzi na Mthibiti Ubora wa Majengo wa Wilaya ya Kyela.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Uliofanyika kata ya Muungano kijiji cha Bukinga Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule Kingamkono, amewapongeza wananchi wa kijiji cha Bukinga kwa kujitoa na Kuchangia kiasi cha Tsh. Milioni 9, na kutoa eneo lenye ukubwa wa Hekali 12.7 kwaajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari katika kijiji hicho.
Aidha Mhe. Katule Kingamkono amewataka Wananchi wa kijiji cha Bukinga, kushirikiana katika kuhakikisha wanasafisha Eneo hilo kwakutoa Majani ili eneo liwe safi kwaajili ya utekelezaji wa mradi wa serikali.
Pamoja na hayo Mhe. Katule Kingamkono ametumia wasaa huo kuwakumbusha vijana kuchangamkia fursa kwani kuanzishwa kwa mradi huo kunatengeneza fursa za ajira kwa wakazi wakijiji cha bukinga na vijiji jirani.
Vilevile Mhe. Katule Kingamkono Amempongeza Mhe. diwani wa kata ya Muungano Lugano Kingdom mwambete kwa kuonesha juhudi za dhati, za kuwapambania wananchi wa kata ya Muungano mpaka juhudi hizo kuzaa matunda.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Muungano Mhe. Lugano Kingdom Mwambete, amefurahishwa sana na juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu hassan, kwa kuwasikiliza wananchi wake na kuwatekelezea mahitaji yao kwa wakati.
Pamoja na hayo, Mhe. Lugano Mwambete, Ameongeza kwa kusema; atahakikisha anasimamia mradi huo kwa ukaribu zaidi ili mradi huo uweze kumalizika kwa wakati.
Hata hivyo Bi. Eva Ngosi mkazi wa kijiji cha Bukinga kata ya Muungano ametoa shukrani nyingi kwa Serikali ya awamu ya sita, kwa kuwatatulia watoto wao adha ya kutembea umbali mrefu kwaajili ya kwenda kusoma, ambapo amesema, watoto wao wanakumbana na changamoto nyingi sana ambazo wengine zinawapelekea kuto maliza Elimu.
Mwisho Mhe. Katule Kingamkono amewataka wananchi wa kata ya Muungano, kuwa walinzi wa mali za serikali pindi miradi ya serikali inapo kuja kutekelezwa katika maeneo yao, kwani kufanya hivyo kutasaidia miradi kumalizika kwa wakati.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa