Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase, ameongoza mkutano wa wadau kujadili utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa usalama wa milki za ardhi tarehe 20/6/2024, katika ukumbi wa Songwe view resort uliopo Kata ya Ikimba wilaya ya Kyela.
Mkutano huo umeudhuriwa na Kaimu Katibu tawala mkoa wa Mbeya, Wakuu wa Idara na Vitengo ngazi ya wilaya na mkoa, taasisi za serikali na binafsi, Wahe. Madiwani, katibu wa Mbunge, viongozi wa kimira na dini , Asasi za kiraia, wataalamu wa nyumba na makazi ngazi ya mkoa, Watendaji kata, wawakilishi wa makundi maalumu na wafanyabiashara wilaya ya Kyela.
Aidha Mhe. Mkuu wa wilaya ya Kyela, ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasan, kwa kuleta mradi utakaoleta manufaa kwa wananchi wa wilaya ya Kyela, hasa kwa wamiliki ardhi.
Mradi huu utasaidia kurasimisha maeneo yanayomilikiwa na wananchi na kuyafanya halali. Pia amewashukuru wadau kwa kuhudhuria mkutano huo ili kuweza kujadili utekelezaji mradi wa uboreshaji wa usalama wa milki ardhi katika wilaya ya Kyela.
Samabamba na hayo Mhe. Josephine Manase, amewatoa hofu wananchi wa wilaya ya Kyela kwamba, kama kutakuwa na changamoto zozote zitakazo jitokeza wakati wa mradi huu, zitatatuliwa kwa utaratibu wa muongozo na sheria za nchi.
Nae kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Dkt.Swaumu Kumbisaga, amesema Halmashauri imepokea mradi huo, pia amewashukuru wadau wa mradi huu, kwani mradi utatatua migogoro ya ardhi, hasa kwa wakulima na wafugaji.
Pia wananchi watapata hati milki ya ardhi. Na amewaomba wataalamu wa mradi kuwa na ushirikiano katika utekelezaji wa mradi kwa kuanza kutoa elimu vijijini.
Kwa upande wake Afisa mipango miji mkoa wa Mbeya Alpha Mangula amesema vijiji 90 vitafanyiwa urasimishaji katika halmashauri ya wilaya ya Kyela.
Pia ameeleza vigezo vitakavyomuwezesha mwananchi kufanya urasimishashaji ni pamoja na kua na kitamburisho cha Taifa(NIDA).
Kwa upande wake Tumaini Setumbi ambaye ni afisa maendeleo ya jamii mwandamizi kutoka wizara ya ardhi makao makuu Dodoma amesema wakati wizara ikiandaa nyaraka mbalimbali za kuhakikisha wanapata fedha walitumia miongozo mbalimbali ya kisheria za nyumbani na kimataifa lengo likiwa ni kulinda kuishirikisha jamii husika.
Mradi huo unatarajiwa kuwafikia wananchi katika mitaa ya Ipinda, Mikumi, Itunge, Bondeni A, Bondeni B, Serengeti, na Ndandalo, ambapo kabla ya kuanza utekelezaji wizara inatarajia kuhamasisha wananchi juu ya uelewa wa mradi huo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa