Haya yamesemwa na mwenyekiti wa halmashauri wa wilaya ya kyela mhe. Hunter mwakifuna katika kikao cha waandishi wa habari katika ofisi ya mkurungenzi mtendaji wilaya ya kyela tarehe 29.08.2019, majira ya saa 11:oo asubuhi siku ya alhamisi.
Kutokana na tukio lililofanywa na vijana katika Kata ya Makwale, kijiji cha Mpunguti siku ya jumatano, tarehe 28,08,2019,majira ya saa 5:15 jioni. Vijana ambao walikuwa wanapinga kuzikwa kwa kijana mwenzao aliyejulikana kwa jina la Richard Kamunyoge, aliyefariki ghafla wakati akicheza mpira na kuamini kuwa amekufa kwa imani za kishirikina ( kurogwa) ndio walisababisha uvamizi huo.
Mwenyekiti mh. Hunter Mwakifuna amesema vijana hao walivalia Tisheti za rangi nyekundu walivamia Msafara wa mkuu wa wilaya mhe. Claudia Kitta, akitoka kukagua baadhi ya miradi ukiwepo mradi wa barabara ya Matema. Vijana kwa kuhofia kwa mhe. Claudia kitta kuwaingilia maamuzi yao ya kupinga kuzikwa kwa mwenzao mpaka uchunguzi ufanyike ndipo walipoamua kuziba barabara na kuanza kushambulia msafara kwa mawe.
Pia mwenyekiti Hunter Mwakifuna amesema kutokana na tukio hilo maafisa usalama wawili walipata majeraha kadhaa, lakini Mhe. Claudia Kitta alifanikiwa kuondoka salama katika tukio hilo. Mpaka sasa watu 45 wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.
Aidha mkurungenzi mtendaji Mhe. Polycarp Benedict Ntapanya, amekemea vikali juu ya tukio hilo, amewasisitizia wananchi wa Wilaya ya Kyela kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani ulinzi na usalama umeimarishwa pande zote.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa