Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa leo tarehe 24/08/2024, katika viwanja vya shule ya msingi Kambikatoto wilayani Chunya Mkoani Mbeya, ukitokea mkoani Tabora.
Mwenge wa Uhuru utakimbizwa Halmashauri 7 ukiwa ndani ya mkoa wetu wa Mbeya.
Wilaya ya Kyela tunatarajia kuupokea tarehe 28/08/2024, siku ya jumatano katika eneo la viwanja vya shule ya sekondari KCM kata ya Busale na kufanya mkesha katika viwanja vya TRA kata ya Njisi.
Shime wananchi wa wilaya ya Kyela, tujitokeze katika kuupokea Mwenge wetu kwa bashasha, shangwe, fijo na ndelemo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa