Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Mheshimiwa Katule G. Kingamkono amefanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa wodi ya mama na mtoto tarehe 30/11/2021, katika hospitali ya wilaya ya Kyela.
Mheshimiwa Katule G. Kingamkono Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela,(shati drafti) akiwa na wananchi na viongozi wengine katika mradi wa ujenzi wa wodi ya mama na mtoto.
Akizungumza na baadhi ya wananchi walioungana nae katika zoezi la kukagua mradi huo, Mheshimiwa Mwenyekiti amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ndugu Ezekiel H. Magehema , kwa upendo wake wa dhati katika kusimamia miradi ya maendeleo katika wilaya ya Kyela.
Aidha alisema, "Matamanio ya wanaKyela ni kuona jengo hilo linakamilika ifikapo Januari 2022" kwani kwa kufanya hivyo wananchi hao watatambua thamani yao ya nguvu kazi na fedha walizochangia kwa ujenzi huo.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri amesema, pongezi nyingi ziende kwa wananchi wa Kyela waliokuwa wakihudhuria vikao vya kisheria, na hata kukubaliana kujenga jengo la ghorofa, ili kuepuka kutumia eneo kubwa na kuifanya Kyela kuwa ya kisasa zaidi.
Mwisho Mheshimiwa Mwenyekiti aliwapongeza watalaam wote walioshiriki hadi kuufikisha mradi hatua uliopo, na amewaomba kuanza mapema hatua inayofuata kwa ujenzi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa