Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono amefanya ziara tarehe 21/03/2024 ya kutembelea zahanati na vituo vya afya kwa lengo la kuhamasisha utoaji wa huduma bora.
Katika ziara yake Mhe. Kingamkono ameongozana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Saumu Kumbisaga pamoja na baadhi ya wakuu wa idara na vitengo.
Akizungumza na watoa huduma katika zahanati ya Kata ya Ikolo na Kilasilo Mhe. Mwenyekiti amewataka watoa huduma ya afya kutumia lugha za kuwafariji wagonjwa, kwani lugha nzuri ni faraja kwa mgonjwa na ni sehemu ya tiba kisaikolojia.
Amesema Viongozi wilayani Kyela, hawatamvumilia mtumishi yeyote, ambae atatumia lugha ambazo si rafiki kwa mgonjwa, kwani Serikali ya awamu ya sita imejenga vituo vya afya, zahanati nyingi pamoja na kununua vifaa tiba vya kutosha, lengo ni kumsaidia Mwananchi.
Hivyo amesema, haipendezi kwa Mhudumu yeyote wa afya kuwa na kauli zisizo rafiki kwa mgonjwa kwani kwa kufanya hivyo hawaitendei haki Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ziara za Mheshimiwa Mwenyekiti wa halmashauri zitafanyika kwa takribani wiki mbili, ili kupata fulsa za kuongea na watoa huduma za afya walipo katika ngazi ya vijiji na kata.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa