Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono, amechangia shilingi 500,000/= kwa ajiri ya ujenzi wa vyoo katika shule ya msingi Kijila iliyopo kata ya Nkokwa hapa wilayani Kyela.
Mchango huo ameutoa wakati akifanya mkutano wa hadhara, katika kijiji cha Kijila kata ya Nkokwa, tarehe 11/05/2023 kwa lengo la kuhamasisha ujenzi wa vyoo katika shule hiyo, Kwani vyoo vilivyopo kwa sasa si rafiki kwa matumizi ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.
Aliendelea kusema, Serikali ya awamu ya sita inawakumbuka sana wananchi wake, Hivyo kwa kupitia Halmashauri ya wilaya ya Kyela imetoa milioni 9 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi wa shule ya msingi Kijila.
Aidha amewaeleza bayana wananchi wa Nkokwa kuwa, shilingi milioni 9 haiwezi kukamilisha ujenzi wa vyoo hivyo kwa wanafunzi jinsia ya kike na kiume, hivyo wananchi wa Kijila wanapaswa kuchangia mradi wa ujenzi huo.
Aidha aliwashauri wananchi kukaa kwa pamoja na kuchangia nguvu kazi hata fedha kidogo ili kumalizia ujenzi wa vyoo hivyo.
Pasipokuwa na shaka, Wananchi wa kata ya Nkokwa walihamasika na kukubaliana kuchangia shilingi elfu 10 kwa kila kichwa ili kukamilisha ujenzi huo.
Nae Mhe. diwani wa kata ya Nkokwa Mhe. Hassan Mwambokela amemshukuru Mhe. mwenyekiti kwa hamasa kubwa ya ujenzi wa vyoo katika shule ya msingi Kijila katika kata ya Nkokwa na alichangia shilingi 200,000/= kwa ujenzi wa vyoo.
Pamoja na hayo mheshimiwa Mwenyekiti alipata fulsa ya kutembelea kata ya Ngonga na Katumbasongwe ili kuwapa pole wananchi kwa kukatika kwa mawasiliano baina ya kata hizo mbili baada ya daraja tegemezi kuvunjika.
Mwenyekiti wa halmashauri Katule G. Kingamkono (picha ya juu mwenye kofia) akiwa anaongea na baadhi ya wananchi wa kata ya Katumbasongwe na Ngonga, ambao wamepata adha ya kukatika kwa mawasiliano baada ya daraja la Nsesi kuvunjika.
Hata hivyo serikali kupitia Halmashauri ya wilaya ya Kyela iliweza kupeleka boti kwa haraka ili kusaidia kurejesha mawasiliano baina ya kata hizo mbili kwa muda wakati taratibu za kutengeneza daraja hilo zikiendelea.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa