Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mheshimiwa Katule G. Kingamkono ( Mwenye kofia) amepata fursa ya kutembekea Banda la Halmsahuri ya wilaya ya Kyela, linalopatikana hapa katika viwanja vya maonesho Kihesa Kilolo Mkoani Iringa, ili kujionea maonesho ya vivutio mbalimbali vinavyopatikana wilayani Kyela.
Wilaya ya Kyela imebahatika kuwa na vivutio vingi vya utalii, ikiwemo Kilambo visima vya maji moto, Mapolomoko ya Maji Mwalalo, Ikato lya Nyerere, Katago, Fukwe za ziwa nyasa Matema, pamoja na vivutio vingine vingi vya kiasili. Tembelea banda letu upate kuyajua yote hayo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa