Akiongea na Wananchi wa kata ya Muungano leo tarehe 19/09/2023, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Katule G. Kingamkono amesema,
Amepata faraja kuona wananchi wengi wamejitokeza katika mkutano, Hii inaonyesha ushirikiano uliopo baina ya wananchi na viongozi.
Pia ametoa salamu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia suluhu Hassan kwamba anawapenda wananchi wa kata ya Muungano.
Aidha amewataka wanaMuungano kuendelea kuungana na kuachana na malumbano ili wafanye maendeleo. Amewapongeza wana Muungano kwa kushirikiana katika kufanya maendeleo.
Pamoja na hayo amesema atakaeikoa kata ya Muungano ni wanaMuungano wenyewe,Pia amesema, hakuna Serikali ambayo inamuuacha mwananchi wake ataabike, hivyo mnapoanza kujenga, kujitoa na kushikamana ili kujenga shule ya Sekondari, Serikali itawaona kwa kujitoa kwenu ili kufanikishaa jambo jema mlilolianza la ujenzi wa sekondari.
" Ili mradi huu uwende na spidi Mtendaji wa kata ni lazima utoe taarifa ya mapato na matumizi kwa kila mwezi, na wananchi wakikosa amani hautaweza kuwasimamia". amesema Mhe. Katule.
Awali Mtendaji wa kata ya Muungano ndugu Rashidi Mwalupembe amesema, wananchi wa kata ya Muungano wameamua kujenga shule ya sekondari, itakayoitwa Ipande Mashariki, na hadi sasa wananchi wamechangia Shs. 7,687500/=.
Nae Mhe. diwani wa kata ya Muungano Mhe. Lugano Mwammbete Amemshukuru Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kuacha shughuli zake na kuongea na wananchi wa kata ya Muunguno, amesema wananchi hawa wameamua kujenga shule yao, kwa sababu, wanafunzi kutoka kata ya Muungano kwenda kata jirani ya Ipande ilipo shule ya Sekondari ni km 2.
Ambapo wakati wa masika njia hazipitiki, Pia wanafunzi kutoka kata ya Muungano kwenda kata jirani ya Nkokwa ni km 7 ambako ni mbali zaidi.
Hivyo wanafunzi wanapata taabu sana kwenda kuoata huduma ya elimu ya Sekondari kutokana na hilo, wananchi wameamua kujenga shule yao ya Sekondari.
Mwenyekiti wa Halamshauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono, amewahamasisha wananchi hao kwa kuwachangia mifuko 20 ya simenti ili kuanza ujenzi huo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa