Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono ametembelea kitongoji cha Nduka kata ya Ngana ili kusikiliza changamoto mbalimbali wanazopitia wakazi wa Kitongoji cha Nduka.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara tarehe 10/11/2023 katika Kitongoji cha Nduka, Mhe. Katule Kingamkono, Amempongeza Mhe. diwani wa kata ya Ngana Mhe. Kajela kwa kukipigania kitongoji cha Nduka, kwani wananchi hao wanapitia changamoto kubwa sana ikiwemo kutokuwepo kwa hospital pamoja na miundo mizuri ya barabara.
Aidha Mhe. Katule Kingamkono amewapongeza wazazi wa kitongoji cha Nduka, kwakuwa na muamko wa Elimu kwa watoto wao, Pia kutambua Umuhimu wa Elimu kwa watoto.
Mhe. Katule Kingamkono ameahidi kuwa bega kwa bega na wananchi wa kitongoji cha Nduka na kuhakikisha na uongozi wa wilaya ili zahanati ijengwe katika kitongoji hicho, kilicho mbali na huduma za afya.
Wananchi wa Nduka katika harakati za kuanza ujenzi wa mradi wa zahanati, wamefyatua tofali elfu 8, Pamoja na kuchanga kiasi cha pesa Tsh Laki 3.
Pamoja na hayo katika harakati za kuunga mkono juhudi za upatikanaji wa zahanati ili kuwakomboa kina mama wajawazito na watoto Mhe. Katule Kingamkono, amechangia kiasi cha shilingi laki 5 na kuahidi kutoa shilingi laki 5 nyingine mara baada ya kupatikana fundi ili ujenzi uanze mara moja.
Vilevile Mhe. Katule, amewataka wananchi katika kitongoji cha Nduka kutokuwa wanyonge kutokana na changamoto zinazowakabili bali kuwa na mshikamano na umoja ili kufikia malengo ya maendeleo, katika kitongoji hicho.
Pamoja na hayo, Mhe. Katule Kingamkono amewataka Wananduka kuongeza juhudi na maarifa kwa kuanzisha vitega uchumi mbalimbali ili kujikomboa na umasikini katika kitongoji cha Nduka.
Akiunga mkono Juhudi zakujikomboa na umasikini katika kitongoji cha Nduka, Mhe. Katule Kingamkono ameahidi kuwaletea vifaranga vya kuku 20 ili kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku pamoja na kuwaletea miche 500 ya miti ya michikichi.
Wananchi wa Kitongoji cha Nduka wamefurahi na wamemshukuru Mhe. Katule Kingamkono kwa kuwatembelea na kuguswa na changamoto wanazopitia katika kitongoji hicho kwani ni viongozi wachache wenye moyo huo.
Mhe. Katule Kingamkono amehitimisha mkutano huo kwa kuwaomba wazazi wa kitongoji hicho kuwaunga mkono watoto wao katika suala la elimu, kwani elimu ndio msingi bora wa maisha ya mwanadamu.
Mwisho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa