Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa Ndg. Maganya Abdul Fadhil Rajab, amefanya ziara ya kukagua Miradi ya maendeleo ikiwa ni kuona kutekeleza wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) tarehe 23/02/2025.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa (Mbeya Girls) Shule ya Sekondari ya Wazazi Ngana,Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela.
Ziara hiyo imeambatana na zoezi la upandaji miti katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Mbeya Girls, kama njia mojawapo ya uhifadhi na utunzaji Mazingira.
Akiwa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana, Ndugu. Maganya ameuagiza uongozi wa Wilaya kusimamia mradi huo na kuhakikisha majengo yaliyobaki yanakamilika kwa viwango bora na Wanafunzi wanapata masomo katika mazingira mazuri.
Aidha akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya wasichana Mbeya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngana kwa nyakati tofauti Ndg.Maganya amewasihi wanafunzi hao kuwa na nidhamu nzuri pamoja na kufanya juhudi katika masomo yao, kujiepusha na vishawishi vitakavyosababisha kutotimiza ndoto zao.
Aidha Ndugu. Fadhil Rajab ameupongeza Uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Kyela Kwakuwajali wazee kwakuweka Madirisha yaliyowekwa Alama kwaajili ya kuwarahisishia Wazee kufahamu mahali wanapotakiwa kutibiwa katika Vyumba vya Wazee.
Ndugu. Maganya ameongeza kuwa sehemu nyingi alikopita Vituo vya Afya vimejengwa vizuri na kuona vyumba vya matibabu kwa ajili ya wanawake na kupumzikia watoa huduma lakini hakuna vyumba vya wazee.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amemshukuru Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi kwa ziara yake ya kukagua Miradi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyela,pia amesema uongozi wa Wilaya utahakikisha unasimamia miradi kwa kufuata vigezo na viwango vilivyopangwa ili kuhakikisha Wananchi wanapata huduma stahiki.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa