Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Pastory Mnyeti, amefanya zoezi la kukabidhi boti za uvuvi 4 za kisasa kwa wavuvi kutoka Mkoa wa Ruvuma, Njombe na Mbeya, zoezi ambalo limefanyika tarehe 15/11/2023 katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela.
Akizungumza wakati wa kukabidhi boti, Mhe. Naibu Waziri amesema, kwa awamu ya kwanza serikali itakabidhi boti 160 nchi nzima, na nyingine zitakuja kwa awamu ya pili, Hivyo kila mwananchi mwenye sifa na uhitaji wa mkopo wa boti hizo anakaribishwa wakiwa aidha ni mtu binafsi, kikundi au kampuni. Kwani serikali inafanya jitihada hizi ili kuinua sekta ya uvuvi wenye tija nchi.
Aidha amewataka wanufaika wa mkopo huo kurudisha marejesho kwa wakati, ili wavuvi wengine wapate fursa ya kukopeshwa boti za kisasa kama hizi zilizokopeshwa sasa kwa awamu nyingine.
Vilevile Mhe. Mnyeti ameongeza kwa kusema, Wizara ya Uvuvi na Mifugo inaendelea kutoa elimu juu ya ufugaji wa samaki katika vizimba na kwa sasa elimu hiyo itaanza kutolewa katika ziwa Nyasa, Pia wizara ina mpango wa kuanzisha Mamlaka za Uvuvi nchini Tanzania, hususani sehemu zote ambazo shughuli za uvuvi zinafanyika, lengo la serikali ni kutaka kuratibu na kusimamia masuala yote yanayohusu uvuvi nchini.
Pia Mhe. Mnyeti amewataka wataalamu kutoka mamlaka ya uvuvi kutoa elimu haraka sana juu ya matumizi ya boti hizo za kisasa, ili wamiliki waanze kuzifanyia kazi mara moja.
Mhe. Alexander Pastory Mnyeti amehitimisha kwa kumpongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kwani hadi sasa Mhe. Rais amegusa sekta zote, kilichobaki ni sisi watumishi kufanya kazi, ili kuhakikisha nchi ya Tanzania inafikia malengo ya kujiinuka kiuchumi duniani.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa