Afisa tarafa wa tarafa ya Ntebela iliyopo katika wilaya ya Kyela bi. Noreen Mwanjela amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Joseph Pombe Magufuli, kwa kuwapelekea mradi wa maji Safi na salama katika kijiji cha Ikombe kilichopo katika kata ya Matema wilayani hapa.
Akizungumza leo tarehe 1/10/2020 kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kyela, bi. Noreen amesema;
Leo ni siku ya kuvunja kamati ya maji ya mpito, iliyokuwa ikisimamia mradi wa maji hapa kijijini Ikombe, Ila amegundua kuwa hakukuwa na mawasiliano mazuri baina ya kamati ya mpito iliyokuwepo pamoja na kamati mpya iliyochaguliwa. Hivyo aliwataka wajumbe wa kamati ya mpito kutoa ushirikiano kwa kamati ya sasa kwani tofauti zao zimeongelewa leo na kufikia muafaka baina pande zote mbili.
Kwa kufanya hivyo aliwataka wajumbe wa kamati, kushirikiana ili kuufanya mradi wao wa maji kusonga mbele. Pamoja na hilo amewataka wafanyakazi wa RUWASA wilayani hapa kuwatembelea Mara kwa mara wanakamati hao ili kuzidi kutoa elimu juu ya uendeshaji wa mradi wa maji.
Aidha akikabidhi cheti na kanuni za jumuia ya watumia maji Ikombe, amewataka wajumbe wa kamati kuzingatia muongozo na taratibu za matumizi ya fedha za serikali, Pia kuzingatia amani na utulivu katika kijiji cha Ikombe kwa wakati wote huu wa kampeni hadi uchaguzi Mkuu, kwani serikali haijalala na itamshughulikia yeyote atakaekuwa chanjo cha kuvuruga amani hapa kijijini.
Nae aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya maji ya mpito ndungu Assa s. Mwanyamaki amesema, yeye amekuwa kiongozi kwa miaka 6, na amekuwa na ushirikiano mkubwa na wajumbe wenzake hadi kuufanya mradi huo kufikia siku ya leo. Hivyo anawaomba wanakamati mpya kuiga mfano wao na wapo tayari kushirikiana kwa lolote ili kuifanya mradi kuwa endelevu.
Ndugu Nazareth P. Mgunda ambae ni mwenyekiti wa kitongoji cha Isumba kijijini Ikombe, ametoa shukrani zake za dhati kwa serikali kwa kuwaletea mradi wa maji safi na salama kwani kabla ya hapo, walikuwa wakitumia maji ya ziwa ambayo ni safi lakini si salama.
Watalaam kutoka serikalini wakiwa katika boti kuelekea kutoa huduma kwa wananchi katika kijiji cha Ikombe.
Habari na Mawasiliano
Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa