Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa, amefungua rasmi Maonyesho ya Biashara ya Kusini International Trade Fair & Festival leo tarehe 14 Septemba 2025 katika Kata ya Matema, Wilaya ya Kyela.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Malisa amewataka wafanyabiashara kuhakikisha usafi wa mazingira muda wote, hususan kipindi chote cha maonyesho hayo. Amesisitiza kuwa kila shughuli itakayofanyika kwenye maonyesho hayo iguse kwa namna moja au nyingine suala la utunzaji wa mazingira.
Aidha, RC Malisa ametoa rai kwa waandaaji wa maonyesho hayo kuhakikisha matamasha na mambo mbalimbali yanayohusisha elimu kwa wananchi yatolewe kwa njia ya mikutano na semina kwa kuandaa kumbi za mikutano, badala ya kila mtu mmoja mmoja kwenda kujifunza kwenye mabanda.
Vilevile, amesisitiza kuwa maonyesho hayo yawe chachu ya kuitangaza Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kupitia zao la kakao. Amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kyela kuandaa eneo maalumu litakalotumika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu zao la kakao kwa undani zaidi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa