Katibu wa Mbunge ndugu Edger Mlaghila akishirikiana na Meneja wa RUWASA Eng. Tanu Deule wamepokea rola 67 na mabomba 80 leo tarehe 28/06/2021, mabomba haya yameletwa kwa lengo la kumalizia mradi wa maji wa kata ya Mababu katika kijiji cha Kilombero.
Akiongea baada ya mapokezi ya mabomba hayo, katibu wa Mheshimiwa mbunge amewaomba wananchi kupokea vizuri miradi hii ya maji ambayo inatekelezwa kwa wakati huu. Pia amesema, kazi za maendeleo zinahitaji nguvu kazi, hivyo popote miradi hii inakopita ni vema wananchi tukajitokeza ili kushiriki shughuli mbalimbali katika miradi hiyo.
Aidha amesema serikali imekuwa na kasi kubwa sana ya utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya yetu, na kwa kuwa wilaya ya Kyela imekuwa na tatizo la maji kwa mda mrefu, anaamini sasa tatizo hili linakwenda kwisha.
Pia katibu huyo wa mbunge ameishukuru sana serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwekeza fedha nyingi za miradi ya maji katika wilaya yetu, Pia amepongeza ushirikiano mkubwa uliopo baina ya ofisi ya Mbunge, Mkuu wa wilaya, pamoja na Ofisi ya mkurugenzi, kwani ushirikiano huu ndio unaoleta maendeleo haya tunayoyaona leo.
Nae meneja wa RUWASA amekili kupokea mabomba hayo , na kuwata wananchi kutambua kuwa, serikali yao inawajari sana na hivyo kuwataka kuwa walinzi wa miradi yote ambayo inakweda kutekelezwa hapa wilani.
"RUWASA MAJI BOMBANI"
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa