Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase akiwa katika kikao cha baraza robo ya nne.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono akiwa katika mkutano wa Baraza la robo ya nne.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Bi. Florah A. Luhala akiwa katika Mkutano wa Baraza la robo ya nne.
Akiongea katika Baraza la robo ya nne la Waheshimiwa Madiwani, lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, 19/08/2923, Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amesema;
Wanakyela tunapenda kutoa salamu nyingi za pongezi na shukrani kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha nyingi ambazo zinatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hapa wilayani.
Amesema tumeendelea kunufaika na miradi ya Elimu ikiwemo mradi wa ujenzi wa shule mpya ya wasichana ya Mkoa inayojengwa katika kata ya Busale ambayo hatua za awari za ujenzi zinaendelea, amesema tumepokea milioni 100 ambazo zitajenga nyumba za walimu katika shule ya sekondari Bondeni kata ya Bondeni, Milioni 500 kwa ujenzi wa shule mpya ya sekondari kata ya Ibanda.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa wilaya amesema tumepewa zaidi ya shilingi bilioni 20 kwa ujenzi wa skimu ya umwagiliaji kata ya Makwale, pia tunazo meli katika ziwa Nyasa, ambazo zinatuunganisha na nchi jirani kibiashara na kusafirisha abiria ndani ya nchi yetu.
"Tumepokea fedha nyingi kwa miradi ya maji, ili kumaliza tatizo la maji wilayani Kyela, shilingi bilioni 7 kwa mradi wa maji kata ya Ngana, mradi utakao hudumia kata zaidi ya mbili na vijiji vyake". Amesema Mhe. Manase.
Pongezi nyingi amezitoa kwa viongozi na wakuu wa Idara na Vitengo kwa kazi nzuri za kukusanya mapato pamoja na ushirikiano.
Awali pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri Katule G. Kingamkono alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la waheshimiwa Madiwani la robo ya nne, Mheshimiwa Katule amesema;
Tunampongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutuletea fedha ambazo zimetuinua na kuanzisha miradi mingi ya maendeleo, ikiwemo zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ujenzi wa shule mpya za msingi 2 na ujenzi wa nyumba vya madarasa katika shule kongwe, tumepewa shilingi milioni 4 kwa ununuzi wa vifaa tiba katika vituo vya afya na zahanati,
Pamoja na hayo amesema, tumeendelea na ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika hospitali ya wilaya, Pia amesema, anaamini ndani ya mwaka huu wa fedha jengo litakamilika na kuanza kutoanhuduma kwa wananchi.
"Tayari tumepokea pesa zaidi ya shilingi milioni 750, itakayotuwezesha kumalizia jengo ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi" amesema Mhe. Katule.
Ametoa pongezi kwa wakuu wa idara, vitengo pamoja na viongozi wote wa wilaya, kwa kusaidia ukusanyaji wa mapato ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 tumekusanya zaidi ya100% , Amepongeza usimamizi mzuri wa matumizi wa mapato hayo, na hatimae wilaya imepata hati safi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa