Haya yamejidhihirisha wazi wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, ziara iliyofanyika kwa takribani Siku mbili tarehe 01 hadi 02/08/2021 hapa wilayani Kyela.
Serikali imeahidi kupeleka umeme kwa kila kijiji ambacho hakijapata umeme hadi sasa katika wilaya ya Kyela, na baada ya kumaliza vijiji vyote serikali itapeleka umeme hadi katika vitongoji vyote vya wilaya zote za Tanzania, haya yote yanafanywa kwajitahada za Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Samia Suruhu Hassan ili kuhakikisha kila mwananchi wa Tanzania anafikiwa na huduma ya umeme. Amesema serikali imeweka mkandarasi atakaemalizia kuingiza umeme katika halmashauri ya Rungwe, Busokelo na Kyela na atakapofika Kyela amemtaka kuwasha umeme katika kijiji cha kingiri kabla ya vijiji vyote vilivyobakia.
Pamoja na hilo amemtaka mkandarasi huyo kuwasajiri wateja wote bure, kwani serikali imepunguza gharama za uingizaji wa umeme kutoka shilingi 380,000 hadi shilingi 27000 na nguzo bure ili kumsaidia mwananchi kupata huduma ya umeme popote nchini.
Kuhusiana na zao la kakao, Mheshimiwa waziri Mkuu amesema serikali yetu ni serikali sikivu, imesikia kilio cha wanaKyela kupitia Mbunge makini wa jimbo la Kyela, Mhe. Ally Kinanasi na kuahidi kulishughulikia zao hilo ili wananchi waweze kufaidika nalo. Hata hivyo Mhe. Waziri Mkuu alisema atafanya kikao na viongozi mbalimbali ili kujiridhisha na utulivu uliopo kwa sasa hapa Kyela na atamuagiza Mhe. Waziri wa kilimo kuja kutoa msimamo juu ya zao la kakao Kyela.
Aidha Naibu waziri wa kilimo Mhe.Hussein Bashe amesema, wameyachukua maagizo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri Mkuu na pia aliwaagiza maafisa kilimo wa halmashauri ya Rungwe, Busokelo na Kyela kuandaa vitalu vya michikichi na kokoa ili kuweza kuwagawia miche wakulima bure.
Serikali italeta kwa wakulima miche 40,000 ya chikichi na kuigawa bure kwa wakulima wa Kyela. Ili kuendeleza na kukuza kilimo cha chikichi hapa wilayani.
Wakati huo huo Mhe waziri Mkuu alipata fulsa ya kutembelea bandari ya Kiwira, na kuitaka kampuni ya Songoro marine, kumaliza haraka ukarabati wa meli ya MV Mbeya ii, ili kurudisha huduma ya usafiri kwa wananchi.
Pia alimuagiza Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Ismail Mlawa kufanya vikao vya ujirani mwema na nchi ya Malawi, ili meli zetu za mizigo ziweze kusafirisha mizingo hadi Malawi, Na kuwasaidia wananchi na wafanyabiashara wa nchi zote mbili kufanya biashara katika mazingira mazuri ya usafiri.
Mwisho Mhe.Waziri Mkuu aliweza kutembelea Chuo cha ufundi studi cha "Kyela Polytechnic College", na kituo cha usafirishaji cha pamoja cha " One Stop Border Post" ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa