Leo nakuletea picha za miradi mbalimbali ambayo imeweza kutembelewa na Waheshimiwa Madiwani wa wilaya ya Kyela, katika robo ya kwanza ya mwaka 2019-2020.
Miradi hii yote ni jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano, ikisaidiana na nguvu za wananchi katika maeneo husika, ambapo miradi hiyo inatekelezwa.
Uanzishwaji wa miradi hii ni jitihada za serikali ya awamu ya tano, katika kuhakikisha wananchi waondokana na umaskini, hivyo Waheshimiwa madiwani kupitia kamati zao za kudumu wametembelea miradi hii ili kutoa ushauri na kuhimiza kasi ya ukamilishaji wa miradi ya wananchi na Serikali ili Mradi M kukamilika kwa wakati.
Picha ya jengo la zahanati inayojengwa katika kijiji cha Kasala.
Waheshimiwa madiwani wakitembelea Ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Kasala, kilichopo katika kata ya Mwaya wilayani Kyela, hadi kufikia hapo zaidi ya shs. Milioni 21,900,00/= zimeshatumika.
Mradi wa ukarabati wa miundo mbinu ya maji lubaga.
Huu ni mojawapo ya mradi ambao umetembelewa na Waheshimiwa Madiwani, mradi huu unafanywa baada ya mkandarasi aliekuwa akijenga barabara kuuharibu, hivyo kufanya ukarabati upya.
Mradi huu unafanyika katika kijiji cha lubaga Kata ya Bujonde wikayani Kyela.
Mradi huu utatumia kiasi cha shilingi milioni 54,560,000/= hadi kukamilika kwake.
Hapa Wahesimiwa madiwani wakitembelea ujenzi wa zahanati inayojengwa katika kijiji cha Kyangala Kata ya Talatala wilayani Kyela.
Ujenzi huu ni kwa nguvu ya serikali ikisaidiana na nguvu ya Wananchi waishio ndani na nje ya kijiji hicho.
Hata hivyo waheshimiwa Madiwawani waliweza kutembelea vituo vya ukusanyaji wa mapato, ziara zilizofanywa ghafla ili kujua utekelezaji wa majukumu katika maeneo hayo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa