Haya yamezungumzwa na Mhe. Naibu waziri wa maji Meryprisca Mahundi alipokuwa katika ziara ya kikazi katika eneo la Mambe Busokelo katika mradi wa maji wa mto Kanga tarehe 31/12/2020.
Mheshimiwa Naibu waziri wa maji amesema chanjo cha maji cha Kanga kinauwezo wa kuzalisha maji lita 15,000,000 ambazo zinauwezo wa kutoshereleza mahitaji ya maji kwa wilaya ya Kyela, Hivyo serikali imeamua kuleta pesa zaidi ya shilingi 3,000,000,000 ili kumaliza tatizo la maji wilaya ya Kyela na ukizingatia wilaya ya Kyela inahitaji maji lita 8,000,000 tu kutoshereza wananchi wote wilayani hapa.
Pia amesema chanjo cha maji cha Kanga group kimefanyiwa utafiti na kubanika kuwa ni moja ya chanjo cha maji ambacho hakitakuwa na mashaka yoyote katika kumaliza adha ya maji wilayani Kyela, kwani hata katika kipindi cha kiangazi chanzo hichi huwa na maji zaidi ya lita 13,000,000. Pia ameiagiza mamlaka ya maji Mkoa wa Mbeya kupitia mkurugenzi wake kuanza kazi mara moja ya maandalizi kuanzia mwezi huu wa kwanza.
Aidha akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kyela Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Kyela Mlaghila Jumbe, amesema sasa kwa mara ya kwanza Kyela tatizo la maji linakwenda kuwa histiria, pia alimwomba Mheshimiwa Naibu waziri asiichoke Kyela, kwani bado hata huko vijijini kunauhitaji wa maji, na alisema kuna baadhi ya vyanjo vya maji vinavyohiyajika kupata nguvu ya sola tu ili kuvuta maji kutoka katika vyanzo na kusambaza kwa wananchi.
Pia Mkuu wa wilaya ya Kyela Mshimiwa Claudia U. Kitta alitoa shukrani zake za dhati kwa mheshimiwa Naibu waziri kwa kufika kwake, na alimwomba kulizingatia ombi lao la uchimbaji wa visima virefu mradi utasaidia watu kupata maji wakati wakiwa wanasubili mradi mkubwa kukamilika, na ombi mradi huo upo mezani kwa Mhe. Waziri wa maji aliepita.
Mwisho Mheshimiwa Naibu waziri aliwapongeza watumishi wote waliofanya uchunguzi wa chanzo hicho na aliwataka kutokulala sasa kwani serikali ya sasa ipo katika utekelezaji wa kutoa huduma kwa wananchi wake kwa haraka na kwa umakini mkbwa sana.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa